Redds
Miss Ilala Dorice Mollel (katikati) akipozi na washindi wenzake.
Kutoka kulia ni mshindi wa pili Alice Isaac na mshindi wa tatu Clara
Bayo.
Redds Miss Ilala 2013 Dorice Mollel(kulia) akiwa na Noela Michael aliyemaliza muda.
Na Mwandishi Wetu
Miss
Tabata Dorice Mollel (22) usiku wa kuamkia jana aliwashinda warembo
wengine 13 kushinda Redds Miss Ilala 2013 katika shindano iliyofanyika
kwenye ukumbi wa Golden Jubilee Tower, Dar es Salaam.
Dorice alimrithi Noela Michael ambaye alishinda taji hilo mwaka jana pia akitokea Tabata.
Dorice alizawadiwa 1.5milioni/-, na mshindi wa pili Alice Isaac (Dar City Centre) alipata 1milioni /-.
Mshindi
wa tatu katika shindamo hilo ni Clara Bayo (Dar City Centre) ambaye
alizawadiwa 700,000/-. Mshindi wanne Pendo Lema (Tabata) alizawadiwa
400,000/- na watano Shamim Mohamed alipata 300,000/-.
Mrembo
Juanita Kabunga kutoka Tabata alizawadiwa 500,000/- baada ya kushinda
Miss Talent na Kabula Kibogoti pia kutoka Tabata alishinda taji la Miss
Rio and Spa na kuzawadiwa 200,000/- na ajira ya kudumu kwenye kampuni
hiyo.
Warembo waliosalia kila moja alipata kifuta jasho cha 200,000/-.
Warembo
hao ni Clara Paul, Anna Johnson, Irene Mwelolo, Rehema Mpanda, Martha
Gewe, Diana Joachim, Natasha Mohamed, Kazumbe Mussa, Kabula Kibogoti na
Juanita Kabunga.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)