MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AKUTANA NA MAMA WA WATOTO WAWILI MAJERUHI WA MLIPUKO WA BOMU LA ARUSHA WALIOLAZWA HOSPITALI YA AGA KHAN JIJINI NAIROBI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AKUTANA NA MAMA WA WATOTO WAWILI MAJERUHI WA MLIPUKO WA BOMU LA ARUSHA WALIOLAZWA HOSPITALI YA AGA KHAN JIJINI NAIROBI


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Aisha Omari (kushoto) Mama wa watoto wawili waanga wa mlipuko wa Bomu la Arusha, Sharifa Jumane (9) na Fatuma Jumanne (8) waliolazwa katika Hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi. Mama huyo alifika kuzungumza na Makamu akiwa jijini Nairobi leo asubuhi, Agosti 1, 2013 kuelezea hali ya watoto, ambapo pia alitoa shukrani zake kwa Serikali inayoendelea kuwahudumia watoto hao. Katikati ni Balozi wa Tanzania, nchini Kenya, Batrida Buriani.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Aisha Omari, Mama wa watoto wawili waanga wa mlipuko wa Bomu la Arusha, Sharifa Jumane (9) na Fatuma Jumanne (8) waliolazwa katika Hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi. Mama huyo alifika kuzungumza na Makamu akiwa jijini Nairobi leo asubuhi, Agosti 1, 2013 kuelezea hali ya watoto, ambapo pia alitoa shukrani zake kwa Serikali inayoendelea kuwahudumia watoto hao. 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages