MAKAMU WA RAIS AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA KUMUAPISHA RAIS WA IRAN - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAKAMU WA RAIS AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA KUMUAPISHA RAIS WA IRAN


IMG_3355 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Kiislam ya IRAN  Mhe.  Al-Akbar Hashemi Rafsanjani  wakati  Makamu wa Rais alipofika kwenye Makazi ya Rais huyo mjini Teheran Iran leo Ogast 05-2013, Makamu wa Rais yupo Nchini Iran kwa ajili ya kuhudhuria kuapishwa Rais Mpya wa Nchi hiyo alieapishwa jana jioni. IMG_3337 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Kiislam ya IRAN  Mhe. Al-Akbar Hashemi Rafsanjani wakati  Makamu wa Rais alipofika kwenye Makazi ya Rais huyo mjini Teheran Iran leo Ogast 05-2013, Makamu wa Rais yupo Nchini Iran kwa ajili ya kuhudhuria kuapishwa Rais Mpya wa Nchi hiyo alieapishwa jana jioni. IMG_3366Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo kutoka kwa maafisa wa Rais mstaafu wa Jamhuri ya kiislam ya Iran alipotembelea makazi ya Rais Al-Akbar Hashemi Rafsanjani mjini Teherani Iran leo Ogast 05-2013. (Picha na OMR Teheran)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Makamu wa Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, jana alikuwa mmojawapo wa wageni mashuhuri katika sherehe za kumuapisha Rais wa mpya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Watu wa Iran  Mheshimiwa  Hassan Rouhani, sherehe iliyofanyika katika makao makuu ya nchi hiyo yaliyopo jijini Tehran. Kabla ya sherehe hiyo ya kuapishwa, Jumamosi Agosti 4, 2013, Mkuu wa Kidini wa nchi hiyo Ayatollah Ali Khamenei alimthibitisha Rais Rouhani na akatumia nafasi hiyo kufafanua kuhusu aina ya mahusianio ambayo Iran inataka kuyaona baina yake na nchi zingine duniani.


Mheshimiwa Makamu wa Rais alikuwa miongoni mwa viongozi wapatao 55 kutoka nchi mbalimbali walioshiriki sherehe hizi huku vyombo vya habari kutokana nchini Iran vikielezea kuwa tukio la jana kwamba ni la kihistoria kwani Iran haikuwahi kuwa na wageni mashuhuri wengi kiasi hicho katika sherehe zake za kuapisha viongozi wa nchi hiyo. Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na Rais aliyemaliza muda wake, Rais Mahmoud Ahmadinejad.


Akihutubia wananchi wa Iran sambamba na wafutiliaji wa siasa za Iran mara tu baada ya kuapishwa, Rais Rouhani alisema Iran inategemea kuwa nchi za ulimwengu wa kwanza zitatafuta suluhu nayo kwa mazungumzo na siyo kwa kutumia vikwazo. Kauli hii alikuwa anaitoa siku moja baada ya seneti ya Marekani kupitisha kwa azimio moja vikwazo zaidi kwa Iran saa chache kabla ya Rais Rouhani kuthibitishwa na Ayatollah Khamenei, Kiongozi mkubwa kabisa na mwenye heshima ya juu katika Iran.


Wachambuzi wa masuala ya kisiasa na kimashirikiano wanaamini kuwa serikali ya Rais Rouhani ambayo aliitangaza mara tu baada ya kuapishwa, itaanza kazi kwa wakati huku ikibadili uelekeo kutoka katika siasa za mrengo wa kushoto na kuwa siasa za kawaida ambazo zitafungua mahusiano zaidi na nchi za Mashariki.


Tanzania ina uhusiano wa siku nyingi na Iran na siku kadhaa za mwisho wa utawala wa Rais Ahmadinajad, Iran ilikubali kuifutia Tanzania deni lake lililokuwepo kwa miaka mingi kwa lengo la kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizi mbili. Pia, Iran imekuwa ikisisitiza ukuzaji wa biashara hasa ya nyama kati yake na Tanzania huku kukiwa tayari na makampuni kadhaa ktoka Iran yanayowekeza katika eneo la Ujenzi.


Katika ziara hiyo Mheshimiwa Makamu wa Rais pia alipata fursa ya kukutana na Rais wa tatu wa Iran Akbar Hashem Rafsanjeni na kufanya naye mazungumzo kuhusu mashirikiano baina ya nchi zetu mbili. Rais Rafsanjeni aliyepata kufika Tanzania mwaka 1996 alisisitiza kuwa kuna mengi ambayo Iran ilipanga kufanya na Tanzania mbayo yalizorota baada ya utawala wake lakini ni imani yake kuwa yataendelea kufanyiwa kazi sasa. Baadhi ya maeneo aliyoyajadili ni katika elimu ambapo katika kipindi chake alianzisha kozi za Kiswahili katika vyuo vya Iran na eneo lingine likiwa la kuwezesha upatikanaji wa viwanda vya Korosho.


Kwa upande wa Mheshimiwa Makamu wa Rais alimueleza Rais Mstaafu Rafsanjeni kuwa, Tanzania inatambua uhusiano wa kihistoria iliyonao na Iran na kwamba ina nia ya dhati kuona uhusiano huo unaimarika zaidi na hasa katika maeneo ya uwekezaji na biashara za pamoja. Rais Mstaafu Rafsanjeni alisema kuwa Iran kwa sasa inakabiliwa na vikwazo kadhaa ambavyo kwa namna moja ama nyingine vimekwamisha baadhi ya mambo ambayo wao kama nchi waliyapanga kuyafanya lakini akafafanua kuwa anaona tuendako kuna nuru hivyo mafanikio ya kutimiza makubaliano baina ya nchi zetu yanaweza kufikiwa.


Msafara wa Mheshimiwa Makamu wa Rais ambao pia uliambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mahadhi Maalim umeondoka leo hapa Tehran kurejea nyumbani. “Tuna mengi ya kujifunza kutoka Iran na uhusiano wetu wetu una kila sababu ya kudumishwa,” alimalizia Mheshimiwa Makamu wa Rais baada ya kuagana na Rais Mstaafu Rafsanjeni na saa chache kabla ya kurejea nyumbani.

Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais

Tehran, Iran

Jumatatu Agosti 05, 2013



<head>
	<title>NEWS; KESI YA WANACHAMA WA CHADEMA YAFUTWA WATUHUMIWA WAACHIWA HURU</title>
	<meta property="og:title" content="NEWS; KESI YA WANACHAMA WA CHADEMA YAFUTWA WATUHUMIWA WAACHIWA HURU" />
	<meta property="og:description" content="








&nbsp;
 watuhumiwa wa Kesi &nbsp;ya ugaidi &nbsp;iliyokuwa inwakabili wanachama wa 
Chadema akiwemo Henry kilewo wameachiliwa Huru Baada ya Kesi Yao kufutwa
 na jaji katika mahakama kuu Huko Tabora&nbsp;

HabAri zaidi itakujia HAPAHAPA KAA nasi&nbsp;

CHANZO ;JAMIII FORUM

" />
	  	<meta property="og:image" content="https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhjDPECJxvBXaPF_s-ubszaTt_oAvMcvS0NpHmMBYZStIt95287nQvmSpQiRFY4_pgp8yDUJm0L0DawnmoT5BdS68k9bZuhYtnNDTr9oXsDT8_KL6O-PLaqTaFcyXiPIegiYDGm5oZHT-pZ/s640/blogger-image-1654245531.jpg" />
  	<meta property="og:url" content="http://networkedblogs.com/NP4CN" />
	<meta property="og:site_name" content="Hisia za Mwananchi" />
	<meta property="og:type" content="article" />
    <style type="text/css"><!--

body, .page_content, .page_table {
	background:#fff;
	color:#666;
	font-family:"lucida grande",tahoma,verdana,arial,sans-serif;
	font-size:11px;
	height: 100%;
	margin:0;
	padding:0;
	width: 100%;
	}
html, body, .height_100 {
	height: 100%;
	overflow: hidden;
}
	
a, a:visited {
	color:#999;
	text-decoration:none;
	}
	
a:hover {
	text-decoration:underline;
	}
	
a.voter img {
	border:1px solid transparent;
	border-radius:2px;
		-moz-border-radius:2px;
		-webkit-border-radius:2px;
	height:20px;
	margin-right:1px;
	width:20px;
	}
	
a.voter:hover img {
	border-color:#0068B7;
	}
	
a img {
  border:0;
  }
	
#logo {
  border-radius:20px;
    -moz-border-radius:20px;
    -webkit-border-radius:20px;
  float:left;
	padding:23px 25px 0 0;
	margin-right:8px;
	background:url(http://static.networkedblogs.com/static/images/logo_v5_small.png) no-repeat 0 -3px;
  }
	
#logo:hover {
  background-color:#fff;
  }
	
/* Common Buttons */

a.bt_primary,
a.bt_tertiary {
	border:1px solid #efefef;
	border-radius:2px;
		-moz-border-radius:2px;
		-webkit-border-radius:2px;
	color:#444;
	display:block;
	float:left;
	font-size:11px;
	margin-right:6px;
	padding:0;
	text-align:center;
	text-decoration:none;
	}
	
	/* IE fix */
	a.bt_tertiary {
	  height:20px;
		width:70px;
	  }
		
	a.bt_primary {
    height:14px;
    }

a.bt_primary:hover,
a.bt_tertiary:hover {
	background-color:#0068B7;
	border-color:#0068B7;
	color:#fff;
	}

a.bt_primary {
	background-color:#a0be59;
	border-color:#a0be59;
	color:#fff;
	margin-left:5px;
	padding:3px 6px;
	width:45px;
	}
	
a.bt_primary.off,
a.bt_primary.off:hover {
	background:#D0E1E5;
	border-color:#ccc;
	border-left:0;
	color:#aaa;
	}
	
a.bt_tertiary span {
	background:url(http://static.networkedblogs.com/static/images/sprite_icons.png) no-repeat 0 -20px;
	display:block;
	padding:4px 1em 0 25px;
	}
	
	/* IE fix */
  a.bt_tertiary span {
    height:20px;
    }
	
a.bt_tertiary span.twitter {
	background-position:0 -60px;
	}
	
a.bt_tertiary span.email {
	background-position:0 -100px;
	}

    --></style>
	<script type="text/javascript" src="http://ajax.googleapis.com/ajax/libs/jquery/1.4.3/jquery.min.js"></script>
  <script type="text/javascript" src="http://static.networkedblogs.com/static/js/primer.js?v=5.8"></script>
	<script type="text/javascript">
        function trackEvent(category, action, label, value) {
          _gaq.push(['_trackEvent', category, action, label, value]);
        }
    </script>
</head>
<body>
	<table cellspacing="0" cellpadding="0" class="page_table">
		<tbody>
			<tr>
				<td height="20" style="background:#F7F9FA;border-bottom:1px solid #ccc;padding:10px 9px 8px;">
				<div style="height:25px;overflow:hidden;">
					<div style="float:right;clear:right;padding-top:2px;">
						<a href="http://feedproxy.google.com/~r/HisiaZaMwananchi/~3/lVlbY95Ck3w/news-kesi-ya-wanachama-wa-chadema.html"
              title="Remove NetworkedBlogs frame"
              style="display:block;padding:3px 25px 3px 0;background: url(http://static.networkedblogs.com/static/images/sprite_icons.png) no-repeat scroll right -400px transparent;"
              >close</a>
          </div>
				
					<a id="logo" href="http://www.networkedblogs.com/" title="NetworkedBlogs.com" target="_blank"></a>
					
					<div style="float:left;width:234px;height:22px;overflow:hidden;">
						<a class="bt_tertiary" href='#' title="Facebook share" onclick="sharePost();return false;"><span class="facebook">Share</span></a>
			            <a class="bt_tertiary" href='#' title="Tweet this" onclick="tweet();return false;"><span class="twitter">Tweet</span></a>
                  <a class="bt_tertiary" href='mailto:?subject=NEWS%3B+KESI+YA+WANACHAMA+WA+CHADEMA+YAFUTWA+WATUHUMIWA+WAACHIWA+HURU&body=Hi,%20I%20thought%20you%20might%20like%20this:%0Dhttp://networkedblogs.com/NP4CN%0D%0D(via%20http://networkedblogs.com%20news)'
                    title="Send by email"><span class="email">Email</span></a>
					</div>
					
					<a class="bt_primary" id="votebutton" href='#' title="Vote up this article">Up</a>
					
					<a class="bt_primary" style="width:auto;"
					   href='#' title="Follow this blog"
					   onclick="follow();return false;">Follow Hisia za Mwananchi</a>

          <div id="divVoters" style="float:left;">
          </div>
				</div>
				</td>
			</tr>
			<tr>
				<td class="height_100">
					<iframe frameborder="0" scrolling="auto" src="http://feedproxy.google.com/~r/HisiaZaMwananchi/~3/lVlbY95Ck3w/news-kesi-ya-wanachama-wa-chadema.html" name="content_iframe" class="page_content"></iframe>
	 			</td>
			</tr>
		</tbody>
	</table>

  <div id="fb-root"></div>
  <script>
    var postAttachment = {"picture": "https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhjDPECJxvBXaPF_s-ubszaTt_oAvMcvS0NpHmMBYZStIt95287nQvmSpQiRFY4_pgp8yDUJm0L0DawnmoT5BdS68k9bZuhYtnNDTr9oXsDT8_KL6O-PLaqTaFcyXiPIegiYDGm5oZHT-pZ/s640/blogger-image-1654245531.jpg", "description": "\n\n\n\n\n\n\n\n\n\u00a0\n watuhumiwa wa Kesi \u00a0ya ugaidi \u00a0iliyokuwa inwakabili wanachama wa \nChadema akiwemo Henry kilewo wameachiliwa Huru Baada ya Kesi Yao kufutwa\n na jaji katika mahakama kuu Huko Tabora\u00a0\n\nHabAri zaidi itakujia HAPAHAPA KAA nasi\u00a0\n\nCHANZO ;JAMIII FORUM\n\n", "link": "http://nblo.gs/NP4CN", "name": "NEWS; KESI YA WANACHAMA WA CHADEMA YAFUTWA WATUHUMIWA WAACHIWA HURU", "caption": "Hisia za Mwananchi"};
    var voterIds = "";

    var userId = 0;
    var userName = '';
    var userProfilePic = '';

    function getUserInfo(callback) {
      if (userName != '' && userProfilePic != '')
      {
        // We already have the data, no need to send a request.
        if (callback) callback();
        return;
      }
      FB.api(
        {
          method: 'fql.query',
          query: 'SELECT name, pic_square_with_logo FROM user WHERE uid = ' + userId
        },
        function (response) {
          userName  = response[0].name;
          userProfilePic = response[0].pic_square_with_logo;

          if (callback) callback();
        }
      );
    }

    function addVoterPictures() {
      FB.api(
        {
          method: 'fql.query',
          query: 'SELECT uid, name, pic_square_with_logo FROM user WHERE uid IN (' + voterIds + ')'
        },
        function (voters) {
          for (i in voters) {
            addUserPicture(voters[i].uid, voters[i].name, voters[i].pic_square_with_logo);
          }
        }
      );
    }

    function addUserPicture(userId, name, profilePic) {
      $("#divVoters").append(" id='aVoter_" + userId + "' " +
        "href='#' onclick='window.open(\"http://www.networkedblogs.com/user/" + userId + "\"); trackEvent(\"Toolbar\", \"View Voter Profile\"); return false;' " +
        "class='voter' " +
        "title='" + name + "'>" +
        "mg src='" + profilePic + "' alt='" + name + "' />" +
        "</a>"

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages