Baadhi ya Wafanyakazi wa kampuni ya Serengeti Breweries wakionesha muonekano mpya wa chupa ya Kibo Gold.
Meneja Miradi endelevu na uwajibikaji kampuni ya bia ya Serengeti Nandi Mwiyombela (Katikati), Meneja wa mauzo wa kanda ya kaskazini Patrick Kisaka (kushoto) na Attu Mynah (kulia) kutoka idara ya mipango wakionyesha mbele ya wasambazaji wa bia na waandishi wa habari aina mpya ya chupa yenye shingo ndefu ambayo bia ya Kibo Gold itapatikana kuanzia sasa, hafla hiyo ilifanyika katika kiwanda cha Serengeti Breweries kilichopo mjini Moshi.
Meneja wa miradi endelevu na uwajibikaji Bi Nandi Mwiyombella akizungumza jambo mbele ya Wanahabari na wageni waalikwa kwenye hafla ya muonekano mpya wa bia ya Kibo Gold
Meneja wa kiwanda cha bia cha Serengeti cha njinpi Moshi Bw. Coleman Hanna (katikati) akibadilishana mawazo na meneja mauzo wa kanda ya kaskazini Bw. Patrick Kisaka (kulia) wakati wa uzinduzi wa muonekano mpya wa bia ya Kibo Gold uliofanyika kiwandani hapo mwishoni mwa wiki iliyopita.
Msambazaji wa kwanza kabisa wa bia za Serengeti mkoa wa Kilimanjaro Mama Kisela, akipokea bia ya Kibo Gold yenye muonekano mpya na ladha ileile kutoka kwa Attu Mynah wakati wa uzinduzi wa muonekano mpya wa chupa wa bia hiyo katika hafla fupi iliyofanyika katika kiwanda hicho wmwishoni mwa wiki.
========= ====== =====
KAMPUNI YA BIA YA
SERENGETI YAFANYA UZINDUZI WA MUONEKANO MPYA WA BIA YA KIBO.
SERENGETI YAFANYA UZINDUZI WA MUONEKANO MPYA WA BIA YA KIBO.
*Sasa Kibo yang’ara katika chupa ya kisasa kabisa*
Kampuni ya bia ya Serengeti leo imezindua muonekano mpya wa bia inayosherehekewa sana mkoani hapa, Kibo Gold. Uzinduzi huu uliofanyika katika kiwanda cha bia cha Serengeti kilichopo Moshi, ulifikia kileleni kwa shughuli murua iliyoandaliwa na kampuni hii na kushuhudiwa na waandishi wa habari pamoja na wadau mbali mbali. Bia hii ya Kibo sasa ina muonekano mpya wa chupa inayoashiria ubora wa kilichopo ndani. Bia ni yenye ubora uleule wenye kiwango cha hali ya juu ila kwa chupa ya rangi ile ile iliyongarishwa na shingo ndefu.
Akiongea kwenye hafla hii Meneja wa miradi endelevu na uwajibikaji Bi Nandi Mwiyombella alisema bia hii ya Kibo Gold imekuwa ikitambulika kwa ubora na ladha nzuri kwa wateja. “Kwa muonekano huu mpya wa chupa ya kisasa, tunaamini wateja wengi watavutiwa na kuipenda zaidi
kwani ni muonekano unaokwenda na wakati. Ubora wa bia hii, unakuwa dhahiri kweli kabisa ukizingatia kwamba inatengenezwa kwa maji yatiririkayo kutoka katika kilele cha juu kabisa cha mlima Kilimanjaro ambapo pia bia inazoa jina lake hili la ‘KIBO’, aliongeza Bi Nandi.
kwani ni muonekano unaokwenda na wakati. Ubora wa bia hii, unakuwa dhahiri kweli kabisa ukizingatia kwamba inatengenezwa kwa maji yatiririkayo kutoka katika kilele cha juu kabisa cha mlima Kilimanjaro ambapo pia bia inazoa jina lake hili la ‘KIBO’, aliongeza Bi Nandi.
Kampuni ya bia Serengeti chini ya kampuni mama ya Diageo, inazingatia kanuni na sheria zilizowekwa na kampuni hii kwenye ubora katika uzalishaji wa bidhaa zote. Muonekano wa bidhaa ni ule unaondena na soko za kimataifa na wa kuvutia.
Kampuni ya bia ya Serengeti inatumia malighafi za kitanzania ili kuleta ubora halisi na vile vile kukuza uchumi wa Tanzania katika sekta ya kilimo.
Kampuni ya bia ya Serengeti inatumia malighafi za kitanzania ili kuleta ubora halisi na vile vile kukuza uchumi wa Tanzania katika sekta ya kilimo.
Tafadhali kunywa kistaarabu. Haiuzwi kwa walio chini ya miaka 18.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)