Na Boniface Wambura, TFF
Kamati
ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) imepitia usajili wa wachezaji wa klabu za Ligi Kuu ya
Vodacom na kumuidhinisha Mrisho Ngasa kuchezea timu ya Yanga baada ya
kukamilisha usajili wake.
Hata
hivyo, Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa imebaini kuwa
Ngasa alisaini mkataba mwingine Simba (katika kipindi ambacho alikuwa
na mkataba na Azam) ambapo anatakiwa kurejesha fedha alizopokea (sh.
milioni 30) pamoja na fidia ya asilimia 50 (sh. milioni 15) ya fedha
hizo kwa Simba.
Kamati
pia imemfungia mechi sita za mashindano (kuanzia mechi ya Ngao ya
Jamii), na anatakiwa awe amelipa fedha hizo ndani ya kipindi hicho cha
kukosa mechi hizo. Akishindwa, hataruhusiwa kucheza hadi atakapolipa
fedha hizo.
Vilevile
Kamati imepitia pingamizi zote zilizowasilishwa kuhusu usajili wa
wachezaji, kukatiza mikataba ya wachezaji na kuzitaka klabu husika ziwe
zimetatua masuala hayo hadi Alhamisi (Agosti 22 mwaka huu).
Kwa
upande wa wachezaji wa kigeni, Kamati imeagiza wasiruhusiwe kucheza
hadi watakapopata Hati za Uhamisho wa Kimataifa (ITC) pamoja na vibali
vya kufanya kazi nchini (work permits).
Kamati
hiyo itakutana tena Ijumaa (Agosti 23 mwaka huu) ili kupata ripoti za
pingamizi ilizoagiza ziwe zimefanyiwa kazi hadi Agosti 22 mwaka huu na
kutoa uamuzi kwa pande ambazo hazikuafikiana.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)