Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta
umefungwa baada ya moto mkubwa kutokea katika uwanja huo mjini Nairobi.
Kwa sasa moto huo umeweza kudhibitiwa
Rais Uhuru Kenyatta amewasili katika uwanja huo
na anatarjiwa kuhutibia waandishi wa habari baadaye. Hadi kufikia sasa
hakuna ripoti zozote za majeruhi .
Mwandishi wa BBC katika uwanja huo amesema kuwa kulikuwa na moshi mkubwa uliotoka katika eneo la kuondokea na kuingilia wageni.
Mamlaka ya uwanja huo imesema kuwa tayari watu waliokuwa katika eneo hilo wameondolewa.
Imesema kuwa baadhi ya operesheni za uwanja huo
zimekatizwa huku ndege zinazoingia katika uwanja huo zikielekezwa kutua
katika viwanja vingine ndege kama vile Entebe, Dar es Salam ,Kigali,
Mombasa na kwingineko nchini Kenya. Baadhi ya safari za ndege kutoka uwanja huo pia zime-ahirishwa.
Mwishoni mwa wiki jana baadhi ya wenye maduka ya
Duty Free katika uwanja huo walifurushwa baada ya serikali kusema kuwa
leseni za wenye maduka zilikuwa zimepitwa na muda.
Hata hivyo chanzo cha moto bado hakijabainika.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)