Julio alisema kwa sasa kikosi cha Simba kipo Musoma kujiandaa na mchezo wa agosti 24 dhidi ya wageni wa ligi hiyo, maafande wa Rhino Rangers ambao walikutana na Simba katika mchezo wa kirafiki na kupigwa mabao 3-1 katika uwanja wao wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Awali Wanalindanda Pamba FC ya jijini Mwanza walikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa msimu uliopita Mombeki aliichezea timu hiyo ligi daraja la kwanza na baada ya hapo Simba walimsajili wakisema ametokea Marekani wakati alikuwa mchezaji wa Pamba ya mwanza na kibaya zaidi waliwaambia wanamsimbazi, lakini hawakujali hata kidogo.
Pamba walisema wanajiandaa kupambana na Simba mbele ya sheria kwani wana haki juu ya mchezaji huyo na Simba walitakiwa kukaa nao ili kuwapatia haki yao ya msingi.
Pia habari za uhakika kutoka ndani ya Simba ni kuwa mshambuliaji Amis Tambwe kutoka Burundi anatarajiwa kuwasili leo tayari kujiunga na kikosi cha Simba kinachojiandaa na msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara.
Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Wekundu wa Msimbazi, Simba wametamba kuanza kwa ushindi wa kishindo kampeni zao za kuusaka ubingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2013/2014 kutoka mikononi mwa watani wao wa jadi, Dar Young Africans kwa kuwafunga maafande wa Rhino Rangers katika uwanja wao wa nyumbani wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora Agosti 24 mwaka huu.
Akizungumza na mtandao wa FULSHANGWE, kocha msaidizi wa Simba, Jamhuri Kiwhelo “Julio Alberto” amesema klabu yao ina kikosi cha kazi ambacho wamekiandaa kwa muda mrefu sana na uhakika wa kufanya vizuri msimu ujao ni mkubwa kutokana na wanandinga wao kuzingatia maelekezo ya makocha kwa kiwango cha juu.
“Simba yetu ni Simba ya luku, tunao wachezaji wengi sana na wazuri, wakichoka hawa na kuishiwa nguvu, tunachaji kama mita ya luku, tunachezesha wengine wakati wale wakipumzika, hakika nawaambieni Simba ya luku ya msimu ujao si mchezo”. Alitamba Julio anayesifika kuwa na maneno mengi.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)