Mfanyakazi
wa Inayojiita kampuni ya kukusanya Ushuru ya MTAA WA OYSTERBAY BEACH
PARKING, ambaye hakutaka kutaja jina lake akiandika risiti ya ushuru wa
maegesho ili kuweka katika moja ya gari lililokuwa katika ufukwe wa Coco
Beach, ili alipwe ushuru wa maegesho hayo kiasi cha Sh. 1000 kila gari.
Mfanyakazi huyo alipohojiwa na mtandao huu alisema kuwa anauwezo wa
kukusanya hadi magari 20 kwa siku jambo ambalo si la kweli kwani kwa
muda mchache tu alishapitia magari zaidi ya hayo.
Na
alipoulizwa zinapopelekwa fedha hizo baada ya kukusanywa alisema ''Mimi
sijui zinapopelekwa kwani mimi ni mfanyakazi tu na
nikishakusanya nampelekea Bosi ndo anajua zinapokwenda, kwa siku naweza
kukusanya ushuru hadi wa magari kama 15 hivi,kwa sababu sipo peke yangu
tupo wengi katika eneo hili lote''. alisema mfanyakazi huyo.
Hata
hivyo baadhi ya watu waliokuwapo ufukweni hapo, walisikika wakin'gaka
kutoa ushuru huo, huku wakimhoji ''Tutoe ushuru wa Parking kwa lipi,
hata usafi tu hamfanyi nyie mnajua kuchukua hela tu, na kwanza
mlishazuiliwa kukusanya pesa hizi bado tu mnaendelea na wizi wenu''.
alisikika akilalama jamaa mmoja
Imeelezwa
kuwa Kampuni hiyo inayojishughulisha na kukusanya ushuru huo,
ilishawahi kuwa na mgogoro kipindi cha nyuma, ambapo wahusika waliwahi
kukamatwa na kufikishwa hadi Kituo cha Polisi na kuzuiliwa kufanya kazi
hiyo, kutokana na kutokuwa na ruhusa ya kufanya hivyo na kwamba
hawatambuliki na Halmashauri wala serikali, lakini wanaendelea kinyemela
na kufanya baadhi ya watu wanaowafahamu kuwagomea kutoa ushuru huo
wanapofuatwa kulipia parking hiyo.
Na hata ukiitazama kwa makini Risiti
hii haionyeshi Adress kamili ya wahusika, haina mhuri wala namba za simu
zaidi ya kuandika jina la Serikali ya Mtaa wa Oysterbay Beach, Sasa
kuna kila haja ya kuwahoji Viongozi wa Serikali ya Mtaa huo ili kujua
Mapato na Matumizi ya ukusanyaji wa Ushuru huu, unaokusanywa kuanzia
Jumatatu hadi Jumapili bila kupumzika na zinapokwenda Fedha hizo.
Hii
ndiyo Risiti yenyewe inayotolewa baada ya kutoa Sh. 1000 kwa
mkusanyaji, ambaye pia anakuwa ameambatana na vijana wawili waliovalia
kiraia Jinzi na Tisheti na makofia ya Sweta, wakimlinda mkusanyaji huyu
mdada na kupiga mkwara kwa anayeonekana kukaidi kutoa Buku.
Mkusanyaji
akiandika Risiti hiyo, ambayo hata akiisha ichana haibaki Kopi yake
kuonyesha kilichoandikwa, Yaani ni Vishina kwa kwenda mbele.
Akienda kuweka risiti katika gari
Akitimiza wajibu wake kuweka katika gari....
Huyu ndiye mkusanyaji wa ushuru katika Fukwe hiyo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)