Waziri
wa elimu na mafunzo ya ufundi Dakta Shukuru Kawambwa amezindua mpango
wa matokeo makubwa sasa huku akiwataka wadau kushirikiana katika kuinua
kiwango cha elimu hapa nchini.
Waziri
huyo amesema tayari chombo cha kufuatilia na kutathmini maendeleo
maendeleo ya mpango huo kimeundwa na kusema ni wakati wa
walimu,wazazi,serikali na wadau wengine kufanya kazi kwa pamoja katika
kufanikisha maendeleo ya elimu.
Amesema
mpango huo utajikita katika maeneo manne ya msingi ambayo ni pamoja na
kuinua hadhi ya elimu ya msingi na sekondari,kuwepo kwa uwazi kutoa
motisha na uwezeshaji kwa watendaji wake.
Aidha
naibu Waziri Phillip Mulugu yeye akiwa na dhamana ya kusimamia ukaguzi
na elimu ngazi ya msingi hadi vyuo vya ualimu amesema atahakikisha
ufanisi kwa walimu na wasimamizi wa elimu hapa nchini.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)