Mwanamuziki
Diamond Platnum akimkabidhi funguo ya gari aina ya Toyota Funcargo
mwanamuziki mkongwe nchini mzee Muhidin Gurumo kama zawadi yake kwa
mkongwe huyo wa muziki baada ya kustaafu rasmi kuimba muziki, Diamond
alitoa zawadi hiyo kwa Gurumo katika hafla yake ya uzinduzi wa video
yake mpya ya wimbo Nomber One aliyoirekodi huko Afrika Kusini ikigharimu
kiasi cha dola elfu 30.000 zaidi ya milioni arobaini za Tanzania, Video
hiyo imetengenezwa kwa viwango vya kimataifa na itaweza kumtangaza
vyema kijana huyo wa kitanzania katika ulimwengu wa muziki hasa
kimataifa, Hafla hiyo imefanyika kwenye hoteli ya Serena Dar es salaam
na imehudhuriwa na wasanii pamoja na waigizaji wa filamu na watu maarufu
mbalimbali Mzee
Muhidin Gurumo akimshukuru Diamond kwa kumzawadia gari jambo ambalo
kwake ni kama ndoto kwakuwa amestaafu akiwa hana usafiri “Yaani sijui
hata mke wangu nikimwambia atanielewaje manake ni jambo la kushangaza
kwangu” Alisema mzee Gurumo Diamond akimuongoza mzee Gurumo kwenda kumuonyesha gari Diamond akimuonyesha Mzee Gurumo gari Akimuelekeza jambo baada ya mzee Gurumo kuingia kwenye gari
Diamond akizungumza machache kushukuru mashabiki wake na watu mbalimbali waliomsaidia kufikia hapo alipo Diamond na madansa wake wakitumbuiza katika hafla hiyo Wasanii mbalimbali pamoja na MaDJ walikuwepo katika hafla hiyo hapa ni Dully Sykes na MawanaFA wakiwa na baadhi ya MaDJ Maurice
Njowoka kutoka Cocacola wa pili kutoka kushoto na Mwanamuziki AY wa
tatu kutoka kushoto pamoja na wadau wengine wakiwa katika hafla hiyo
Mwigizaji Jaquiline Wolper naye alitia timu Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka akiwa na mama yake Diamond Wadau mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo Mzee Gurumo akihojiwa na waandishi wa habari Hawa
marafiki zangu wakakumbushia miaka kadhaa waliyofunga ndoa kwa
kulishana mishikaki ilipendeza katikati ni Nancy Sumari akishuhudia Kulia ni Irene Uwoya kushoto Salma Msangi Kushoto AY na Salama Jabir wakipiga story na wadau mbalimbali Kutoka kulia ni Raymond Kigosi, Irene Uwoya na JB wakiwa katika hafla hiyo.Picha Na Fullshangwe Blog
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)