BAADHI YA WANANCHI WAMUIBUKIA DKT. KAWAMBWA KATIKA MKUTANO WA UZINDUZI WA “MATOKEO MAKUBWA SASA” “BIG RESULTS NOW” - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

BAADHI YA WANANCHI WAMUIBUKIA DKT. KAWAMBWA KATIKA MKUTANO WA UZINDUZI WA “MATOKEO MAKUBWA SASA” “BIG RESULTS NOW”

SONY DSC MARIA DAUDI akilia kwa uchungu huku akisaidiwa na wasamaria wema nje ya ukumbi  wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam,  lengo lake lilikuwa kumtaka waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi  Dkk. Shukuru Kawambwa atoke ili kumueleza shida yake, ambapo nyumba yake ilivunjwa kupisha ujenzi wa  wa chuo cha Afya cha muhimbili (MUHANS) huko Kibamba –Mlonganzilo,

SONY DSC MARIA akigalagala chini huku Msamalia mwema akijali kusaidia kumuinua SONY DSC MMOJA wa wananchi hao akionesha moja ya nakala walizokabidhiwa ili kupatiwa malipo yao. SONY DSCMMOJA wa watu wa kundi hilo akifafanua jambo kwa waandishi wa habari
PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE DAR ES SALAAM
Lakini hakutaka jina lake litajwe ,  ”Waziri ameamua kutukimbia wakati anajua wazi kuwa tumekuja hapa ili atutatuliye kero zetu lakini yeye anaamua kutokea mlango wa nyuma hivi kweli tunajenga taifa la namna gani kama waziri mwenye dhamana unaogopa wananchi wako kuwapa ukweli”. Alisikika akiseme

Mtu huyo alidai mwezi wa saba mwaka jana walilazimishwa kuvunjiwa nyumba zao bila kupewa taarifa mapema hatua iliyowafanya kwenda kwa mkuu wa mkoa ili kupatiwa ufumbuzi wa tatizo lao,  lakini mpaka hii leo bado hawajapatiwa maelezo ya kueleweka zaidi ya kuzungushwa kila kukicha,

“Ndugu mwandishi sisi kama unavyotuona tuko hapa toka asubuhi , kwanza tuliambiwa twende wizarani tulipofika huko tukaambiwa waziri hayupo ameenda katika mkutano huko viwanja vya Gymkana na ndipo tukaamua kuja kumuona, lakini mpaka sasa hatumuoni huyo waziri”. alisema mtu huyo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages