ARSENAL 1 VS 2 GALATASARAY: DROGBA AKUMBUKIA ENZI ZAKE, AWAFUMUA ARSENAL MAWILI NA KUTWAA KOMBE LA EMIRATES - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

ARSENAL 1 VS 2 GALATASARAY: DROGBA AKUMBUKIA ENZI ZAKE, AWAFUMUA ARSENAL MAWILI NA KUTWAA KOMBE LA EMIRATES

On target: Drogba scored a late double to clinch the Emirates CupKama kawaida rafiki wa nyavu: Drogba alifumania nyavu mara mbili na kutwaa taji la kombe la Emirates  
Spot on: Drogba sends Wojciech Szczesny the wrong way Drogba akimpeleka sokoni kipa wa Arsenal, Wojciech Szczesny 
Remember me? Drogba celebrates after the final whistleMnanikumbuka? Drogba akishangilia baada ya kipenga cha mwisho cha mwamuzi
Opener: Walcott watched his cross-come-shot give Arsenal the leadUfunguzi wa karamu ya mabao: Walcott akiandika bao la kuongoza kwa klabu yake ya Arsenal
Smiles all round: Walcott celebrates with his Arsenal teammatesFuraha tupu: Walcott akishagilia na wenzake
Return home: Emamanuel Eboue (right) captained Galatasaray on his return to former club ArsenalAmerudi nyumbani: Emamanuel Eboue (kulia) alikuwa nahodha wa Galatasaray akiwa amerufi nyumbani katika klabu yake ya zamani ya Arsena
Disappointment: Arsenal manager Arsene Wenger looks on during his side's defeatDaah! hata kakombe haka kananishinda:  Kocha wa Arsenal,  Arsene Wenger akitazama vijana wake wakiburuzwa.
 
Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com

Didier Drogba “Tembo” amekumbukiza enzi hizo akiwa ndani ya jezi ya Chelsea akiifunga Arsenal baada ya nyota huyo mwenye miaka 35 kwa sasa kuifungia klabu yake ya  Galatasaray ya Uturuki mabao mawili kwenye ushindi wa mabao 2-1 katika mechi ya fainali ya kombe la  Emirates na kutwaa taji hilo.

Kiukweli mechi hiyo ilikuwa ya kirafiki zaidi na haikuwa na thamani yoyote katika msimu, lakini Drogba ameonesha tena umwamba wake wa kuwafunga vijaba wa Arsene Wenger kwani alifanya kazi hiyo mara nyingi zaidi wakati ule akicheza ligi kuu soka nchini England.

Kocha wa Arsenal, mzee Wenger alionekana akilaumu sana kama mechi hiyo ni muhimu mno baada ya kumfuata na kumfokea kamisaa wa mechi hiyo Andre Marriner kutokana na kitendo cha mwamuzi wa kati wa mechi hiyo, Jon Moss  kutoa mkwaju wa penati kufuatia beki wake 

Ignasi Miquel  kumfanyia madhambi mshambulaiji huyo raia wa Ivoru Coast.
Kikosi cha Arsenal:  Szczesny, Jenkinson, Sagna, Mertesacker, Gibbs (Miquel 69), Arteta, Ramsey, Oxlade-Chamberlain, Cazorla (Zelalem 61), Walcott, Sanogo (Giroud 61)
Goli: Walcott 38

Wachezaji wa akiba: Martinez, Koscielny, Podolski, Akpom
Kikosi cha Galatasaray;  Muslera; Semih, Riera, Chedjou, Eboue, Melo (Sarioglu 66), Engin Baytar (Gulselam 32),Altintop (Colak, 45), Amrabat, Elmander (Drogba 45)Umut Bulut (Sneijder 45)

Wachezaji wa akiba: Nounkeu, Balta, Kazim-Richards, Kilic, Kurtrlus, Iscan
Mabao:  Drogba pen 79, 88
Mwamuzi: Jon Moss

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages