Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha akizungumza
machache kabla ya ufunguzi rasmi wa mkutano huo. Anayeonekana pembeni ni
Mhe. John Kijazi, Balozi wa Tanzania nchini India.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akifungua rasmi Mkutano wa
Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (Joint Permanent Commission-JPC)
kati ya Tanzania na India unaofanyika katika Hoteli ya Hyatt
Regency-Kilimanjaro kuanzia tarehe 08 hadi 09 2013. Mkutano huo
unaowashirikisha Wadau kutoka sekta mbalimbali za hapa nchini na India
utajadili pamoja na mambo mengine masuala ya ushirikiano katika sekta za
Uchumi, Ufundi, Sayansi na Teknolojia, Elimu, Afya, Utalii, Kilimo na
Nishati na Madini.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya India, Mhe. Preneet Kaur akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.
Meza kuu kabla ya ufunguzi.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na
Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Bw. Omar Mjenga (kulia) akiwa na Mjumbe kutoka India wakati wa Mkutano
huo.
Wadau wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mhe. Kaur (hayupo pichani)
Wadau wengine wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.
Wadau kutoka sekta mbalimbali za hapa nchini wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi huo.
Wadau zaidi.
Wadau kutoka India.
Wajumbe wa Sekretarieti wakati wa mkutano huo.
Mhe. Membe na Mhe. Kaur wakizungumza
na Waandishi wa Habari mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa Tume ya
Ushirikiano kati ya Tanzania na India.
Mhe. Membe na Mhe. Kaur walioketi, katika picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano huo.Picha na Reginald Philip na Olga Chitanda
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)