Pages

WAZIRI NCHIMBI ASHIRIKI MKUTANO WA KIMATAIFA WA TEKNOLOJIA YA KUPAMBANA NA UHALIFU DUNIANI, NCHINI UFARANSA


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akizungumza katika Mkutano wa Teknolojia ya Kupambana na Uhalifu uliofanyika katika Jiji la Lyon nchini Ufaransa hivi karibuni. Waziri Nchimbi alishiriki mkutano huo pamoja na washiriki wengine kutoka nchi mbalimbali duniani.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (katikati) akimsikiliza kwa makini Rais wa Shirika la Kimataifa la Polisi (Interpol), Mireille Ballestrazzi (kushoto) baada ya Mkutano wa Kimataifa wa Teknolojia ya Kupambana na Uhalifu uliofanyika katika Jiji la Lyon nchini Ufaransa hivi karibuni. Kulia ni Meya wa jiji hilo, Gerald Collomb.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Shirika la Kimataifa la Polisi (Interpol) Mireille Ballestrazzi (kushoto) na Kulia ni Meya wa Jiji la Lyon, Gerald Collomb. Waziri Nchimbi alishiriki mkutano huo wa Kimataifa hivi karibuni. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)