Pages

Miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla, itawasili kwa ndege maalum katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere – Terminal one (Air Wing) saa tisa alasiri Julai 20, 2013

Miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla, itawasili kwa ndege maalum katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere – Terminal one (Air Wing) saa tisa alasiri Julai 20, 2013  badala ya saa nne kama ilivyoelezwa hapo awali, waandishi wa habari wanaruhusiwa  kufika kuanzia saa saba Mchana.

Aidha, mara baada ya kuwasili miili hiyo itapelekwa katika hospitali ya rufaa ya Jeshi,  Lugalo, baada ya maandalizi,  miili hiyo itaagwa rasmi kwa heshima zote Julai 22, 2013 kuanzia saa tatu kamili asubuhi  katika viwanja vya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga, Upanga Jijini Dar es Salaam.

Waandishi wa habari mnaombwa kuhudhuria na kufanya ‘Coverage’ katika mapokezi na hatimaye siku ya kuaga miili hiyo ya mashujaa wetu waliopoteza maisha wakitetea amani duniani.
 
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
SLP 9203, Simu:  0783 309963
Email: ulinzimagazine@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)