Pages

WASANII WA WA KIZAZI KIPYA BONGO FLAVE NA WASANII WA FILM KUFAIDIKA NA SEMINA YA ELIMU YA TEHAMA

Kampuni ya Fahamu inayojihusisha na utoaji wa elimu Tehama( ICT) kwa shule za msingi jijini Dar es Salaam, imeamua kuingia ndani zaidi katika kutoa elimu kwa shule za msingi kwa kushirikiana na wasanii wa muziki wa kizazi kipya bongo freva na wasanii wa filam nchini

Akizungumzia umuhimu wa utoaji wa elimu hiyo ya TEHAMA kwa shule za msingi Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Bwana Mustafa Rubunda alise ameona kuna umuhimu wa kutoa mafunzo hayo kwa watoto wa shule za msingi kuanzia darasa la pili hadi la saba hii ni kutokana na
changamoto ya mabadiliko ya kisayansi na teknolojia amba vijana hao watakuwa na uwezo wa kiubunifu pamoja na kibiashara.

Pia alisema mafunzo hayo yatawafanya wanafunzi kujua teknolojia nini,umuhimu wa habari,matumizi ya mawasiliano,huwa wepesii wa kuelewa na kuwa wabunifu hii itawafanya wanafunzi kuendana na mfumo wa Sayansi na Teknolojia itakayowawezesha  kuingia katika ushindani zaidi na wanafunzi wenzao wa Afrika mashariki,na Duniani kwa ujumla

Mstafa alisema kuwa ili kuhakikisha lengo linakamiliaka Kampuni yake ya Fahamu imeamua kuandaa semina kwa wasanii mbalimbali zaidi ya 100, ambao wataongozwa na Msanii mkongwe Inspector Haorun aka babu,ambaye ndiye Mwenyekiti wa TEHAMA CLASS,na mwakilishi wa wasanii.

Semina hiyo inategemea kufanyika Mwezi huu jijini Dar es Salaam, ambapo itawajumuisha wasanii ,wanafunzi wa sekondari, pamoja na wa Vyuo Vikuu  lengo la kuwa jumuisha katika semina ni kuona umuhimu wa kuweza kuwasaidia wadogo zao katika kuhakikisha wanakuwa watumiaji wa
TEHAMA ambayo sasa ndiyo iliyobeba Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,

Kulingana na uzoefu ambao tayari Fahamu Company  kutokana na kutoa mafunzo kama hayo kwa shule za msingi za Mapinduzi na Rutihinda zilizopo Kigogo katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, alisema kuwa watoto watapata fursa ya kusoma kwa bidii kwani hata wenzao wamekuwa na morali mkubwa wa kujifunza masomo hayo.

Kwa upande wa serikali kupitia TAMISEMI, wamekuwa bega kwa bega kwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Fahamu Campany kwa ajili ya kutoa elimu hiyo kwa watoto wa shule za msigi nchini.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)