HATIMAYE wale Wanawake wawili
walionaswa na madawa ya kulevya Afrika kusini wametambuliwa kuwa
ni mabinti wa KITANZANIA ..
Mabinti hao wanadaiwa kuingiza
shehena ya dawa za kulevya zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8
nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania.
Akizungumza na mwandishi wetu jana,
Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya,
Geofrey Nzoa, alisema haijafahamika wanawake hao wanatoka mikoa gani.
Kamanda Nzoa aliwataja wanawake hao
kuwa ni Agnes Jerald (MASOGANGE) ambaye alisema hajapiga hesabu ya umri
wao, ila alizaliwa mwaka 1988 kwa maana hiyo ana umri wa miaka 25 na
Melisa Edward ambaye alisema amezaliwa mwaka 1989 kwa maana hiyo atakuwa
na umri wa miaka 24. Wawili hao bado wanaendelea kuhojiwa na polisi wa
Afrika Kusini.
Alisema Jeshi la Polisi Nchini kwa
upande wake linaendelea kufanya uchunguzi kubaini kama dawa hizo
walitoka nazo wapi na pia linawasaka watu ambao watakuwa ndiyo wamiliki
wa dawa hizo.
Jumapili iliyopita mtandao huu
ulipata taarifa za kukamatwa kwa dawa za kulevya aina ya Crystal
Methamphetamine zenye thamani hiyo nchini Afrika Kusini wakati
zikisafirishwa kutoka Tanzania.
Taarifa hizo zilionyesha kuwa
wanawake wawili walikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Oriver Tambo uliopo eneo la Kempton Park siku ya Ijumaa wiki iliyopita
wakitokea Tanzania.
Wanawake hao walikamatwa na maofisa
wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini wakiwa na masanduku sita ambayo
yalipokaguliwa yalikutwa na takribani kilo 150 za dawa hizo ambazo pia
zinajulikana kama ‘Tik’ zikiwa na thamani ya bei ya mtaani ya Randi
milioni 42 sawa na Sh. bilioni 6.8.
Baada ya kukamatwa na dawa hizo
wanawake hao walikabidhiwa polisi. Tukio hilo linatoka takribani wiki
moja baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Juni 28, mwaka huu kutangaza
kuwa tatizo la dawa za kulenya hivi sasa ni janga la kitaifa nchini.
Alisema kumekuwa na wimbi kubwa la
Watanzania wanaojiingiza katika biashara haramu ya dawa za kulevya ndani
na nje ya nchi na kwamba, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita,
watuhumiwa 10,799 walikamatwa kwa kujihusisha na dawa hizo.
Pia alisema katika kipindi hicho,
Watanzania 240 walikamatwa katika nchi za Brazil, Pakistan na Afrika
Kusini, na hivyo kuharibu taswira ya nchi na kusababisha Watanzania
wasio na hatia kupata usumbufu na masharti magumu wanapotaka kusafiri
kwenda nchi mbalimbali duniani.
Pinda alisema mwaka huu pekee
kumekuwa na ukamataji mkubwa wa dawa za kulevya katika eneo la kimataifa
la Bahari ya Hindi karibu na Tanzania.
Alisema hivi sasa mikate, maandazi na askrimu zinazouzwa kwenye shule za msingi, zinawekwa dawa za kulevya.
Alisema vitendo hivyo vinafanya
vijana wengi wa shule za msingi na hata sekondari kuwa na tabia za
ajabu, ikiwamo kuingia darasani wakiwa na kiatu kimoja mguuni, mkufu
wenye nyembe na kidani chenye nyembe kifuani.
Melezo Kwa hisani ya Nipashe.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)