TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Dar es Salaam, Julai 18, 2013 – Tigo
Tanzania leo imezindua promosheni kabambe iitwayo “Miliki Biashara Yako”
inayolenga kuwainua wateja wake kiuchumi kwa kuwapatia fursa ya
kushinda usafiri wa Bajaji 60 kwa muda wa miezi miwili ambapo kila siku
mteja atajishindia Bajaji moja.
Akitangaza promosheni hiyo katika
mkutano na wanahabari, Meneja Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga alisema,
“Tigo inatambua jukumu lake tulionao katika kuboresha maisha ya
Watanzania, na kwa sababu hiyo tumeamua kuzindua promosheni ya aina hii
kwa ajili ya kugusa zaidi maisha ya watu. Kwa mara nyingine tena
tunawapa wateja wetu sababu ya kutabasamu wakiwa na Tigo kwa kuwapatia
nafasi ya kumiliki biashara yao wenyewe kupitia promosheni hii ya
“Miliki Biashara Yako”. Hii ni nafasi yakipekee ambapo wateja wetu
watapata fursa ya kuwa wajasiriliamali, kujipatia kipato, kutoa ajira,
pamoja na kutoa huduma ya usafiri wenye gharama nafuu kwa jamii.”
Wateja wa Tigo wanaweza kujishindia
Bajaji moja kila siku kwa muda wa siku 60 kwa kuongeza vocha ya Tsh
1,000 tu kwa siku. Ili kuhakikisha kuwa wateja wengi wanafurahia
promosheni hii, mteja hahitaji kuweka vocha ya Tsh 1000 kwa mkupuo mmoja
ili kushiriki, anaweza kuongeza salio kidogo kidogo hadi kufikisha
kiasi cha Tsh 1000 kwa siku na kuweza kuingia kwenye droo. Vile vile
mteja anaweza kuongeza salio mara nyingi awezavyo ili kujiongezea nafasi
zaidi ya kujishindia Bajaji. Pamoja na hayo, ili kuwapatia urahisi
zaidi wateja, bado mteja anaruhusiwa kuongeza salio pitia namna zote
zile ikiwemo Tigo Rusha, Tigo Pesa au kwa vocha ya kawaida.
“Tunaamini kwamba promosheni hii
itawapatia wateja wetu sababu nyingine yakutabasamu. Wateja 60
watakaopatikana washindi watajinyakulia Bajaji mpya kabisa ambapo
wataweza kuzitumia kuanzisha biashara zao wenyewe. Biashara ya Bajaji ni
biashara yenye faida sana, kwa siku mmiliki wa Bajaji anaweza kuingiza
kipato cha kati ya Tsh 25,000 mpaka Tsh 30,000 kwa siku, sawa na Tsh
900,000 kwa mwezi, ambayo ni Tsh 10,800,000 kwa mwaka,” alielezea
Mpinga.
Bw. Mpinga alisema kwamba kila Bajaji
ina thamani ya Tsh 6,700,000. “Tayari Tigo imechukua jukumu la kulipia
leseni ya barabara (road license) na bima ya Bajaji. Kwahiyo mteja
atakuwa amebakiwa na jukumu la kuja kuchukua Bajaji yake na kuanzisha
biashara yake mara moja,” alimalizia Mpinga.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)