Askari
wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakiwa wamebeba jeneza la Koplo
Mohamed Juma Ali aliyeuawa Daafur katika harakati za kulinda amani chini
ya Kikosi cha Umoja wa Mataifa (Unamid) baada ya kuwasili kwenye
Uwanja wa Ndege wa Zanzibar.
Askari
wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakiwa wamebeba jeneza la Sajent
Shaibu Shehe Othman aliyeuawa Daafur katika harakati za kulinda amani
chini ya Kikosi cha Umoja wa Mataifa (Unamid) baada ya kuwasili kwenye
Uwanja wa Ndege wa Zanzibar.
Baadhi
ya Wanajeshi wakiwa wamebeba Majeneza ya Maiti za Marehemu Sajent
Shaibu Shehe Othman na Koplo Mohamed Juma Ali waliofariki Daafur katika
harakati za kulinda amani chini ya Kikosi cha Umoja wa Mataifa, mara
baada ya kuwasili kiwanja cha ndege cha Zanzibar.
Mke
wa marehem Sajent Shaibu Shehe Othman mwenye Juba jeusi akiwa
ameshikiliwa na ndugu na Askari kutokana huzuni alokuwa nayo mara baada
ya kuwasili mwili wa Mume wake.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar
………………..
Miili
ya Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ waliouawa Darfur wiki
iliyopita Sajent Shaibu Shehe Othuman wa Mpendae na Koplo Mohamed Juma
Ali wa Kwarara imekabidhiwa leo kwa familia zao mara baada ya kuwasili
katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zanzibar.
Marehemu
hao wawili wenye Asili ya Zanzibar ni miongoni mwa Askari saba wa JWTZ
waliuawa walipokuwa wakilinda amani chini ya Umoja wa Mataifa na Afrika
UNAMID,huko Darfur. Miili
ya marehemu hao imewasili majira ya saa 9 alasiri kwa ndege ya JW 90 34
aina ya Boing ikitokea katika Hospitali ya JWTZ Lugalo Jijini Dar es
Salaam.
Mara
baada ya kuwasili Uwanjani hapo Miili ya Marehem hao ilipokelewa na
Katibu mkuu Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Khalid Mohamed Salum
akifuatana na Mwenyeji wake Bregedia Jeneral Kamanda wa Bregedi ya Nyuki
Sharif Sheikh Othuman Viongozi wa Vyama na Serikali,Wanafamilia pamoja
na Wananchi kwa ujumla. Aidha
huzuni ziliendelea kutanda kwa ndugu na Jamaa waliofika kupokea maiti
hizo za
Wapiganaji wa Amani ya Dunia chini ya mwamvuli wa UNAMID. Kwa
mujibu wa Taarifa kutoka Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Shughuli za
Mazishi zitafanyika kesho saa nne za asubuhi katika makaburi ya
Mwanakwerekwe nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Aidha shughuli hiyo ya Mazishi itaambatana na taratibu za kijeshi zitakazofanyika Makaburini hapo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)