Ndugu Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Napenda nichukue fursa hii kuwajulisha rasmi
kwamba Nchi yetu imepata heshima ya kutembelewa na Waziri Mkuu wa Thailand ambaye
atawasili Nchini tarehe 30/07/2013.
Ziara hii ni ya kikazi (state visit) na atawasili katika Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Kumbukumbu ya Mwalimu J. K. Nyerere majira ya saa 6:30 mchana
na kulakiwa na mwenyeji wake Mhe. Rais wetu mpendwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete
akifuatana na Viongozi mbalimbali wa Kitaifa na Mkoa.
Ndugu
Wananchi,
Baada ya kuwasili Mhe. Waziri Mkuu wa Thailand
atakagua gwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili yake na pia atapata fursa ya
kukagua vikundi mbalimbali vya ngoma ambavyo vitakuwa vikitumbuiza na kutoa burudani
kwa Mgeni wetu na msafara wake.
Ndugu
Wananchi,
Mgeni wetu baada ya kukagua vikundi vya ngoma na
burudani ataondoka kuelekea Ikulu kupitia barabara ya Nyerere, Railway,
Gerezani, Sokoine Drive hadi Ikulu. Akiwa Ikulu atasaini mikataba mbalimbali kati
ya Serikali ya Tanzania na Thailand. Usiku atashiriki katika dhifa maalumu
iliyoandaliwa na Mwenyeji wake.
Ndugu
Wananchi,
Tunaomba radhi kwamba barabara hizi nilizozitaja
zitafungwa kwa muda kupisha misafara ya Viongozi wetu Wakuu watakaoelekea Uwanja
wa Ndege wa Kumbukumbu ya Mwalimu J. K.
Nyerere kumlaki Mgeni wetu hususan barabara ya Nyerere kuanzia saa 6.00 mchana
hadi saa 7.30 mchana.
Ndugu
Wananchi,
Tarehe 31/07/2013 Waziri Mkuu wa Thailand
atatembelea Mbuga za Wanyama za Serengeti.Tarehe 01/08/2013 atarejea Dar es
Salaam na kuagwa rasmi katika Uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere na kuendelea na
ziara yake huko Uganda.
Ndugu
Wananchi,
Kama ilivyo ada tunaombwa kumlaki mgeni wetu kwa
shangwe na bashasha katika maeneo yote atakayopita.
Asanteni kwa kunisikiliza.
Saidi
Meck Sadiki
MKUU WA MKOA
DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)