Wachezaji
mbalimbali wa Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Satrs' ambao wanasakata
kabumbu ndani ya nchi wakijifua katika Uwanja wa Taifa wa Mandela uliopo
Nambole nchini Uganda. Stars ipo nchini Uganda na kesho inataraji
kushuka katika dimba la uwanja huo kumenyana vikalina The Crenes ya
Uganda kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa
Ndani CHAN.
Moja
ya mikakati ya Taifa Stars kwenye mechi ya kesho (Julai 27 mwaka huu)
dhidi ya Uganda kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Tatu za Afrika kwa
Wachezaji wa Ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini
ni kushambulia kwa muda mwingi wa mchezo.
Kocha
Kim Poulsen amesema maandalizi ya Taifa Stars jijini Mwanza kwa ajili
ya mechi hiyo ambayo Uganda inaongoza kwa bao 1-0 yalikuwa mazuri,
lakini mabao ni muhimu hivyo watashambulia bila kusahau kulinda lango
lao.
“Unapocheza
mechi za aina hii za nyumbani na ugenini, huku mwenyeji akiwa anaongoza
mabao yana maana kubwa katika mechi. Mabao yanabadili mchezo na pia
wachezaji kifikra,” amesema Kim akizungumza na waandishi wa habari
kwenye hoteli ya Mt. Zion ambayo Stars imefikia.
Amesema
katika mechi ya kwanza walitengeneza nafasi nyingi lakini
hawakuzitumia, hivyo wamekuwa wakifanya mazoezi ya kushambulia, jinsi ya
kutengeneza nafasi, na jinsi ya kumalizia.
“Hivyo
tuko hapa (Kampala) kwa ajili ya kufunga, ni lazima tufunge ili tuweze
kuendelea na mashindano. Lakini ngome yetu nayo ni lazima iwe makini ili
kutoruhusu bao,” amesema Kim na kuongeza kuwa kikosi chake cha kwanza
ni lazima kitakuwa mabadiliko kutoka na Mwinyi Kazimoto kuingia mitini
na Shomari Kapombe kwenda kwenye majaribio Uholanzi.
Amesema
angalau kutakuwa na mabadiliko kwa kuingiza sura mbili mpya katika
kikosi cha kwanza, na kuongeza kuwa wachezaji wanafahamu umuhimu wa
mechi hiyo kwani timu ikienda kwenye Fainali za CHAN itakuwa manufaa
kwao binafsi.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imefanya mazoezi ya
mwisho leo jioni Uwanja wa Mandela ulioko Namboole ambao utatumika kwa
ajili ya mechi hiyo kesho.
Mechi
hiyo itaanza saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki na
itachezeshwa na waamuzi kutoka Madagascar wakiongozwa na Kanoso Abdoul
Ohabee wakati mwamuzi msaidizi namba moja ni Andirvoavonjy Pierre Jean
Eric. Mwamuzi msaidizi namba mbili ni Jinoro Velomanana Ferdinand huku
Andriamiharisoa Hubert Marie Bruno akiwa mwamuzi wa mezani (fourth
official). Kamishna wa mechi hiyo namba 38 ni Ismail Kamal kutoka
Ethiopia.
Stars
inatarajiwa kupangwa hivi; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, David Luhende,
Aggrey Morris, Kelvin Yondani, Athuman Idd, Salum Abubakar, Frank
Domayo, John Bocco, Amri Kiemba na Mrisho Ngasa.
KAKA BLOG YAKO NI NZURI SANA KWA MAANA YA KWAMBA INATOA HABARI NZURI NA ZENYE UHAKIKA.
ReplyDeleteTATIZO NI KWAMBA UNAPOFUNGUA INACHUKUA MUDA SANA KUFUNGUKA NA PIA INAKATA KATA SANA.
NAAMINI UTALIFANYIA KAZI JAMBO HILI
(MFAKI mIKIDADI)
Asante ndugu yangu kwa maoni yako mazuri sana na ni kweli kabisa swala hili linashughulikiwa na wataalamu wetu kuhakikisha tatizo hili halijirudii tena na kuondoa usumbufu kwa Wasomaji wetu. Na kuhusu Kuchelewa Kufunguka Mara nyingi huwa network inapokuwa slow kwa msomaji basi ndio huwa huchelewa kufunguka lakini Pia tunalifanyia kazi hilo kuona hata pale network inapokuwa Ipo vizuri haichelewi kufunguka. Asante Sana Kwa Maoni yako na Yote tunayafanyia Kazi.
ReplyDeleteJosephat Lukaza
Lukaza Blog Admin
+255 712 390 200
E-mail:josephat.lukaza@gmail.com