January Makamba - Mbunge wa Bumbuli
Yaliyojiri Mponde, Bumbuli:
Tarehe 26 Mei 2013, wakulima wa Chai Bumbuli waliazimia kumkataa
mwekezaji/mbia kwenye kiwanda chao cha Chai Mponde ambaye wanaamini
alikuwa anawadhulumu. Pia waliazimia kwamba viongozi wao wa wakulima wa
Chai ambao wameshindwa kusimamia maslahi yao na kujali matumbo yao tu,
waondoke. Vilevile, waliamua kuuza chai yao kwenye viwanda vya jirani na
hivyo kiwanda cha Mponde kufungwa. Na katika kipindi chote hiki
kumekuwa na utulivu wananchi wakisubiri suluhu ya matatizo yao.
Jana, Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto waliamuru
kiwanda kifunguliwe hata kwa mtutu wa bunduki na leo wakapelekwa askari
polisi wakiwa na silaha. Katika kulazimisha kiwanda kifunguliwe wananchi
wamepigwa na watu watano wamejeruhiwa. Kabla ya polisi kwenda hakukuwa
na ghasia yoyote, watu walikuwa wanaendelea na shughuli zao kama
kawaida. Kitendo cha kupigwa wananchi kimewaudhi sana wananchi na
kimeniudhi sana na mimi, wanauliza kwanini inatumika nguvu kubwa kiasi
hiki pahala ambapo hapakuwa na fujo na kwanini inatumika nguvu kubwa
kiasi hiki kumlinda mwekezaji ambaye wananchi kwa kauli moja walimkataa -
tena walimkataa kwa amani bila fujo. Bahati mbaya au nzuri, ni
mwekezaji huyu huyu ndiye aliyekuwa na matatizo na wakulima wa chai kule
Lupembe, Iringa ambao walilazimika kuvamia kiwanda na kukichoma moto.
Sisi hatukuamua kufanya hivyo kwa kuwa sio sahihi.
Nimeongea na
IGP kwamba kuwe na restraint. Watu wetu huwa sio watu wa fujo. Hata
hivyo, watu wakiwa na hisia kwamba wanaonewa wanaweza kufanya chochote.
Naelekea huku kuungana na wananchi wangu, kama ni kupigwa tupigwe sote.
Tarehe 26 Mei 2013, wakulima wa Chai Bumbuli waliazimia kumkataa mwekezaji/mbia kwenye kiwanda chao cha Chai Mponde ambaye wanaamini alikuwa anawadhulumu. Pia waliazimia kwamba viongozi wao wa wakulima wa Chai ambao wameshindwa kusimamia maslahi yao na kujali matumbo yao tu, waondoke. Vilevile, waliamua kuuza chai yao kwenye viwanda vya jirani na hivyo kiwanda cha Mponde kufungwa. Na katika kipindi chote hiki kumekuwa na utulivu wananchi wakisubiri suluhu ya matatizo yao.
Jana, Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto waliamuru kiwanda kifunguliwe hata kwa mtutu wa bunduki na leo wakapelekwa askari polisi wakiwa na silaha. Katika kulazimisha kiwanda kifunguliwe wananchi wamepigwa na watu watano wamejeruhiwa. Kabla ya polisi kwenda hakukuwa na ghasia yoyote, watu walikuwa wanaendelea na shughuli zao kama kawaida. Kitendo cha kupigwa wananchi kimewaudhi sana wananchi na kimeniudhi sana na mimi, wanauliza kwanini inatumika nguvu kubwa kiasi hiki pahala ambapo hapakuwa na fujo na kwanini inatumika nguvu kubwa kiasi hiki kumlinda mwekezaji ambaye wananchi kwa kauli moja walimkataa - tena walimkataa kwa amani bila fujo. Bahati mbaya au nzuri, ni mwekezaji huyu huyu ndiye aliyekuwa na matatizo na wakulima wa chai kule Lupembe, Iringa ambao walilazimika kuvamia kiwanda na kukichoma moto. Sisi hatukuamua kufanya hivyo kwa kuwa sio sahihi.
Nimeongea na IGP kwamba kuwe na restraint. Watu wetu huwa sio watu wa fujo. Hata hivyo, watu wakiwa na hisia kwamba wanaonewa wanaweza kufanya chochote. Naelekea huku kuungana na wananchi wangu, kama ni kupigwa tupigwe sote.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)