SHUJAA WA TANZANIA ALIYEFIA DARFUR RODNEY NDUNGURU AZIKWA KWAO SONGEA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

SHUJAA WA TANZANIA ALIYEFIA DARFUR RODNEY NDUNGURU AZIKWA KWAO SONGEA


 Asikari wa JWTZ wakiwa wamebeba mwili wa Rodney Ndunguru
Aliye kaa katikati ni mama wa marehemu Rodney Ndunguru
 Askari wakiwa wamebeba mwili wa marehemu Rodney Ndunguru wakati wakielekea  katika makaburi ya Mjimwema
 Umati wa watu uliojitokeza katika mazishi ya Rodney Ndunguru katika makaburi ya  mjimwema jana
 Mwili wa Rodney Ndunguru ukiingizwa katika kaburi
 Mama wa marehemu Rodney Ndunguru akiweka taji katika kaburi la mwanaye
---------------------------------------
Na Cresensia Kapinga,Songea.


SIMANZI ,Vilio,majonzi  vimetawala wakati wa mazishi ya askari wa Jeshi la Wananchi Rodney Ndunguru wa kikosi cha makomando cha 92 KJ Ngerengere mkoani Morogoro ambapo mamia ya wakazi wa Mkoa wa Ruvuma wakiwemo askari wa Jeshi la wananchi ambao walihudhuria mazishi yaliyofanyika jana kwenye makaburi ya Mjimwema Manispaa ya Songea.

Katika mazishi hayo ambayo yaliongozwa na Paroko wa kanisa katoriki jimbo kuu la Songea parokia ya Mjimwema padre Noel Duwe ambaye wakati  akiendesha ibada ya mazishi aliwaonya Watanzania kutochezea amani  na kwamba utulivu walionao watanzania unahitajika kulindwa kwa namna ya aina yeyote na si vinginevyo.

Padre Due alisema kuwa kwa wale wote wanaotaka kuchezea amani na utulivu tulionao wanapaswa kukemewa kwa nguvu zote kwa kuwa watanzania hatujazoea vurugu wala umwagaji wa damu jambo ambalo lilionekana kuvuta hisia kwa watu waliofika kuomboleza msiba hu.

Aidha Padri Due alimfagilia waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano Mizengo Pinda kwa kauli yake aliyoitoa Bungeni kuwa kuwa jeshi la Polisi lihakikishe kuwa linawadhibiti watu wanaoleta fujo kwa kupiga na kwamba kauli yenye agizo hilo inapaswa kuungwa mkono kwa nguvu zote badala ya kuibeza kwa kuwa hivi sasa watu wengi wamekuwa wakidharau vyombo vya Dola  wakizani kuwa serikali haipo.
Kwa upande wake  Kaimu wa Brigedi ya kanda ya kusini Kanari George Msongole alieleza kuwa taarifa ya kifo cha Rodney ilipokelewa muda mfupi baada ya kifo chake na kuwa Jeshi la wananachi linaungana  na familia ya marehemu katika majonzi na msiba mzito.

Kwa upande wake msemaji wa Familia ya Marehemu Rodney Ndunguru amesema kuwa  familia imepata pengo kubwa kwa kuondokewa na kijana wao ,na ameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kuisaidia  ili waweze kujengewa nyumba ambayo itwasaidia kwa kuishi mama yake mzazi na mjane.
Alisema kuwa Rodney Ndunguru amefariki akiwa na miaka takribani miaka saba kazini na akiwa na umri wa miaka 28 ambapo kimsingi kifo chake kimeacha pengo kubwa katika famila kwani katika uhai wake ilikuwa farja kwa ndugu na jamaa.
Rodney Ndungu amezikwa saa 10:45 jioni kwenye makaburi ya mjimwema ambako mamia ya wakazi ya mkoa wa Ruvuma walihudhulia akiwemo mwakilishi wa mkoa wa Ruvuma Saidi Mwambungu ambaye ni katibu tawala ya wilaya ya songea Joseph Kapinga na kwamba mazishi yaliendeshwa kijeshi ambapo askari wote walikuwa wamevaa sare huku wakifunga vitambaa vyeusi kwenye mikono yao. 

habari kwa hisani ya demashonews.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages