SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LINALOSHUHULIKIA ELIMU SAYANSI NA UTAMADUNI (UNESCO) LAKABIDHI VIFAA KWA IDARA YA HABARI ZANZIBAR - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LINALOSHUHULIKIA ELIMU SAYANSI NA UTAMADUNI (UNESCO) LAKABIDHI VIFAA KWA IDARA YA HABARI ZANZIBAR

01Mkurugenzi wa Shirika la kimatifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni Vibeke Jense katikati akimfahamisha kitu Mkurugenzi wa Tume ya Utangazaji Omar Chande mara baada ya makabidhiano ya vifaa mbalimbali vya Idara ya Habari Maelezo, kulia Waziri wa Habari Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk.Hafla hiyo ilifanyika  Wizara ya Habari Kikwajuni mjini Zanzibar.02Waziri wa Habari Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk, akimkabidhi zawadi ya mlango  Mkurugenzi Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni Vibeke Jense, huko Ofisini kwake Kikwajuni Mjini Zanzibar. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo-Zanzibar).

Na Miza Othman –Maelezo Zanzibar                     



Shirika la Kimataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO limeikabidhi vifaa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar vyenye thamani ya Shilingi Milioni 46 ili kuijengea uwezo Wizara hio.




Vifaa hivyo ni pamoja na Kamera mbili, Lenzi mbili, Digital Recorder 7, Vipaza sauti viwili, TV moja, pamoja na Mashine 2 za kutayarishia vipindi.



Akikabidhi vifaa hivyo Mkurugenzi wa UNESCO Tanzania Bi Vebeke Jense amesema lengo la kuletwa vifaa hivyo ni kuijengea uwezo Wizara hiyo ili kuleta mabadiliko hasa katika upande wa  tasnia ya habari.



Baada ya Makabidhiano hayo Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk amelishukuru Shirika hilo kwa kuwa karibu na Wizara yake na kuahidi Vifaa hivyo vitatumika ipasavyo ili kutimiza lengo lililokusudiwa.



Waziri Mbarouk amesema iwapo Wafanyakazi watavituza Vifaa hivyo na kuvifanyia kazi ipasavyo hapana shaka mabadikliko katika wizara hiyo yataonekana hasa ikizingatiwa kuwa ni vifaa vya kisasa.



Amesema kwa muda Mrefu Idara ya Habari Maelezo imekuwa na upungufu wa Vifaa katika kukabiliana na majuku yake ya kila siku na kwamba upatikanaji wa Vifaa hivyo itakuwa ni suluhu ya tatizo hilo.



Kwa upende wake Mkurugenzi wa Tume ya Utangazaji Omar Chande amesema itakuwa ni jambo jema iwapo Vifaa hivyo pia vitatumika katika kuandaa habari za vijijini badala ya mijini pekee.



Aidha amefahamisha kuwa baadhi ya vifaa vinatarajiwa kufika siku za karibuni ili kuiwezesha Idara ya Habari Maelezo kuwa ya kisasa na kutimiza maelengo yake.



Msaada huo wa Vifaa vyenye thamani ya Milioni 46 umekuja kufuatia ahadi iliyotolewa na Shirika la UNESCO kwa Idara ya Habari kuiwezesha kupata Vifaa ambavyo vitasaidia katika kuendeleza majukumu yake ya kila siku.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages