Waziri
wa Fedha Dk. William Mgimwa akisisitiza jambo juu ya tozo la kodi
katika laini za simu wakati alipokutana na waandishi wa habari leo
jijini Dar es Salaam. (Picha na Frank Shija – Maelezo)
Na. Eliphace Marwa (MAELEZO)
Serikali yawataka wananchi kutokuwa na wasiwasi kuhusiana na mpango wa ukusanyaji wa kodi ya laini za simu.
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha Dk. William Mgimwa alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Mgimwa
amesema kuwa Serikali inaendelea kukutana na wadau mbalimbali ili
kujadili na kupokea mapendekezo kuhusiana na dhamira ya Serikali kutoza
kodi kutoka katika laini za simu.
Aliongeza
kuwa Serikali ina nia njema ya kuongeza mapato yake ili kuongeza kasi
ya kutoa huduma za msingi kwa wananchi wake hususani wa vijijini.
“Lengo
hasa la kodi hii ni kuboresha huduma za msingi vijijini kama umeme,
maji na barabara ambazo ni duni sana vijijini, hata hivyo tunafanyia
kazi mapendekezo mbalimbali ya wananchi na wadau wenye mitazamo
mbalimbali” alisema Dk. Mgimwa.
Aidha
Dk. Mgimwa amesema kuwa hivi karibuni amekutana na chombo cha watoa
huduma za mawasiliano (MoAT) nakujadiliana nao na kuwaahidi kuwa
mapendekezo yao yatafanyiwa kazi.
Mkutano
huo umekuja baada ya wadau mbalimbali kutoa malalamiko juu ya uwepo wa
tozo ya kodi ya laini za simu ambapo mmiliki wa laini ya simu atatakiwa
kulipia shilimgi 1000 kila mwezi mara kodi hiyo itakapo anza kutozwa.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)