Luis Suarez akifanya mazoezi na kikosi cha majogoo wa jiji baada ya kuwasili nchini Australia jumamosi ya wiki iliyopita
Suarez alifanya mazoezi AMMI leo hii na kuonekana ana morali kubwa katika kibarua cheka katika klabu ya Liverpool
Amefika na kuwapa hai: Suarez baada ya kuwasili Melbourne jumamosi usiku
Mashabiki walijipanga mitaani wakati Suarez na klabu yake ya Liverpool ilipokuwa inawasili hotelini
Morali ya juu: Brendan Rodgers akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mechi dhidi ya Melbourne
Nahodha aliyetukuka Anfiled, Steven Gerrard pia atakuwepo katika kikosi cha Liverpool
Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Mshambuliaji
hatari wa Liverpool, Luis Suarez anatarajia kuichezea klabu yake kwa
mara ya kwanza katika mchezo wa pili wa maandalizi ya ligi kuu soka
nchini England mjini Melbournekeshokutwa tangu afanye kitendo kibaya
cha kumng`ata beki wa Chelsea Branislav Ivanovic.
Suarez
aliwasili Australia jumamosi ya wiki iliyopita akitokea mapumzikoni na
sasa yupo na kikosi cha Brendan Rodgers, huku kocha huyo akisisitiza
kuwa nyota wake atabakia Anfield.
Mechi
hiyo ya kesho kutwa meneja wa majogoo wa jiji anatarajia kumpanga
mshambuliaji huyo raia wa Uruguay ambaye hajatulia kwa sasa klabuni
kuongoza safu ya ushambulizi dhidi ya Melbourne Victory katika dimba la
MCG, lakini kabla ya mechi hiyo Rodgers anatarajia kuzungumza na Suarez
kuhusu hatima yake ya baadaye klabuni hapo.
Suarez
ambaye amekuwa gumzo katika hekaheka za usajili, akihusishwa na mpango
wa kutaka kuihama klabu yake, huku Arsenal wakiwa mstari wa mbele
kuitaka saini yake kwa ada ya uhamisho ya pauni 40, lakini hali
aliyoionesha wakati akiwasili Austaria inabadili mawazo ya wengi
hususani baada ya kukataa kuongea na waandishi wa habari juu ya maisha
yake ya msimu ujao.
Wakati
huo huo kocha wake Rodgers alisisitiza kuwa matarajio yake ni kuwa
Saurez atabakia Anfield msimu ujao na klabu yake haina mpango wa
kumuuza.
Kuelekea mchezo wa kesho kutwa dhidi ya Melbourne Victory, tayari mpaka sasa tiketi 90,000 zimeshauzwa
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)