Rais wa Marekani Barack Obama akiwahutubia wafanyabiashara jana jijini Dar es salaam juu ya mpango wa Nchi yake wa kufungua
milango ya ushirikiano na uwekezaji kwa Nchi za Afrika Mashariki katika
sekta mbalimbali na hivyo kuongeza kiwango cha bidhaa ya Afrika
Mashariki zinazoingia nchini Marekani.
Rais wa Marekani Barack Obama
akiwa katika mkutano jana jijini Dar es salaam wa kujadiliana na
watendaji wakuu(CEO) wa Makampuni mbalimbali yaliyowekeza Afrika juu ya
kuimarisha fursa za ushirikiano kati ya Marekani na Afrika katika
uwekezaji kwenye sekta mbalimbali za maendeleo.Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es Salaam
---
Na Eleuteri Mangi—MAELEZO.Dar es salaam
Serikali
ya Marekani imeahidi kufungua ukurasa mpya kwa Nchi za Afrika Mashariki
kwa kuongeza uwekezaji katika sekta mbalimbali ili kuinua uchumi wan
chi hizo.
Kauli
hiyo imetolewa jana mjini Dar es salaam na Rais Barack Obama kwenye
hotuba yake kwa wafanyabiashara wakati wa ziara yake ya siku mbili
nchini Tanzania.
Alisema
kuwa hatua hiyo inalenga kuongeza kiwango cha bidhaa kutoka Nchi za
afrika Mashariki kuingia nchini Marekani na hivyo kuimarisha ushirikiano
wa kibiashara na kiuchumi kwa manufaa ya pande zote.
“Sasa
ni wakati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwekeza nchini Marekani ili
kuongeza mauzo yake nchini Marekani hadi ifike asilimia 40,” alisema
Rais Obama.
Aliongeza
kuwa pia ushirikiano huo unapaswa kuboresha utoaji wa mizigo katika
bandari ya Dar es salaam na Mombasa kwenda nchi zisizo na bandari ili
kuinua uchumi wa eneo hilo kwa kupunguza muda wa mizigo kukaa bandarini.
Akizungumzia
hotuba ya Rais Obama Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye viwanda nchini
(CTI) Felix Mosha alipongeza hotuba hiyo kwa kufungua ukurasa mpya kwa
nchi za Afrika na Marekani kwa kuonyesha kuwa wakati wa kutegemea
misaada umepitwa na wakati badala yake ni kushirikiana katika uwekezaji.Katika mkutano huo kiasi cha wafanyabiashara 170 walihudhuria mkutano huo .
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)