Meneja wa bia ya Serengeti Allan Chonjo(katikati) akiongea na wana
habari wakati wa kumtangaza mshindi wa droo ya tatu ya Winda na Ushinde
ambaye ni Bi Blanca Mariki, katika ofisi za Kampuni ya Bia ya Serengeti jana jijini Dar es Salaam, akiwa pamoja na wadau wengine wa droo hiyo Meneja mauzo wa Push Mobile Rugambo Rodney(kulia) na Afisa mwandamizi kutoka PWC Daniel Nnko (kushoto).
Meneja wa bia ya Serengeti Allan Chonjo akiongea
na mshindi wa droo ya tatu ya Winda na Ushinde kwa njia ya simu, huku
akishuhudiwa na Afisa Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Bahatinasibu
Tanzania Emmanuel Ndaki(wa kwanza kushoto), Afisa mwandamizi kutoka PWC
Daniel Nnko(wa pili kushoto) na Meneja mauzo wa Push Mobile Rugambo
Rodney(kulia), katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jana
katika ofisi za Kampuni ya Bia ya Serengeti jijini Dar es Salaam.
Allan Chonjo ambaye ni Meneja wa bia ya Serengeti akiongea na Blanca Mariki(mshindi wa droo ya tatu ya Winda na Ushinde) kwa njia ya simu katika ofisi za Kampuni ya Bia ya Serengeti jana jijini Dar es Salaam.
Akitoa maelezo kwa wana habari kuhusiana na droo ya tatu ya Winda na
Ushinde Meneja wa bia ya Serengeti Allan Chonjo akiwa na wadau wengine
walioshiriki katika droo hiyo jana katika ofisi za Kampuni ya Bia ya
Serengeti jijini Dar es Salaam
Mfanya biashara ndogondogo kutoka Morogoro
atangazwa mshindi wa kitia cha 1,000,000 kutoka kampuni ya bia ya Serengeti kwa
promosheni hiyo.
11 Julai
2013, kampuni ya bia ya Serengeti imetangaza mshindi wa droo ya mwisho ya
promosheni ya Winda na Ushinde ambae amejinyakulia kitita cha milioni moja
baada ya kuchezesha droo yake ya tatu na ya mwisho. Droo hiyo ilichezeshwa
katika ofisi za kiwanda hicho jijini Dar es Salaam huku ikishuhudiwa na mhakiki
kutoka katika bodi yamichezo ya Bahati
Nasibu.
Baada ya kupokea simu Blanca Mordest Mariki(30) anayefanya biashara
ndogo ndogo kutoka Morogoro alionesha furaha yake na kubaki bumbuwazi kwa
furaha. “Nimefurahi sana kuwa mshindi wa promosheni hii ya Winda na Ushinde
kutoka katika kampuni ya Bia ya Serengeti. Na najivunia kuitumia bia ya
serengeti kwani ndio bia niipendayo na nawapongeza sana kampuni ya Serengeti
kwa kuanzisha mashindayo haya” Pamoja na ushindi huu mkubwa nimeshajishindia
bia za bure za Serengeti mara mbili, pamoja na hela taslimu shilingi 10,000
mara nne ambazo huwa natumiwa kupitia njia ya simu”. Alisema mshindi huyo.
Akiongelea promosheni hii meneja wa kinywaji cha bia ya Serengeti Allan
Chonjo alisema “promosheni hii ni ya kipekee na mpaka sasa watanzania wengi wameshajishindia
bia za bure na pesa taslimu ambazo ni shilingi 10,000 na100,000/= na pia washindi wetu wakubwa wa droo ya
kwanza na ya pili walijishindia milioni moja kila mmoja. Mshindi wa droo ya
kwanza alitoka Kilimanjaro na mshindi wa pili alitoka Dar es Salaam na wote waliipongeza
sana kampuni ya bia ya Serengeti kwa kuwasaidia wateja kwani wameinua uchumi
wao kupitia ushindi wao wa promosheni hii”.
“Lengo
la kampuni yetu ni kuendeleza umoja na mshikamano na wateja wetu kwa kuutambua na kuuthamini mchango
wao kwani wao ni muhimili mkubwa katika kukuza na kuendeleza bia yetu ya
Serengeti. Promosheni hii inaendelea mpaka mwisho wa mwezi Julai na kumalizika
kwa promosheni ya Winda na Ushinde ni mwanzo wa mengine mengi yanayotolewa na
kampuni ya bia ya Serengeti kwa ajili ya wateja wetu”. Aliongeza meneja huyo.
Tafadhari kunywa kistaarabu na ni maalum kwa 18+
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)