Msomaji wa Quran tukufu katika
mashindano ya kitaifa, Seif Salim Said ambaye ni mremavu wa macho
akisoma wakati wa fainali zake leo
Na Mwandishi Wetu
MASHINDANO ya kitaifa ya kuhifadhi Quran tukufu yamemalizika leo, huku walemavu wa viungo wakiwa kivutio cha aina yake, kwa
kuonyesha maajabu.
Walioshangiliwa na hata kuwatoa machozi watazamaji walikuwa ni Ummy
Kuluthumu Swaleh Saidi kutoka Pemba, ambaye hakuwa na miguu wala mikono
pamoja na Seif Salim Said ambaye ni mlemavu wa kuona na kusikia,
waliweza kusoma vizuri bila kubabaika huku wakiwapita hata wale
waliokuwa na viungo kamili.
Mashindano hayo yalimalizika jana Dar es Salaam katika ukumbi wa
Diamond Jubilee ambapo yalihusisha washiriki 72 kutoka Tanzania Bara na
Visiwani. Walemavu hao pamoja na wengine sita, walizawadiwa fedha taslim pamoja na fimbo za kuwawezesha kutembea.
Nafasi ya mshindi wa kwanza kwa wavulana ilikwenda kwa Abdul Hamid na
msichana alikuwa Suria Ally Bakari ambao kwa pamoja walipewa Bajaji na
fedha taslim sh. 500,000.
Washindi wa mashindano hayo yaliyoandaliwa na Eshe Sururu Foundation,
yaligawanywa katika makundi matano, kwa upande wanawake na wanaume,
huku washindi wengine wakiondoka na pikipiki, baiskeli, vyereheni na
fedha taslim.
Katibu wa kamati ya maandalizi, Issah Ramadhan Mohamed alisema kuwa
madhumuni ya kuandaa mashindano hayo ni kuibua ari kwa vijana wa kiislam
waweze kusoma Quran Tukufu kwa mustakabali wa maisha mema.
Alisema yalishirikisha wasichana 38 na wavulana 34 ambapo kila upande
alitoka mshindi wa kwanza hadi wa tatu na yaligawanywa kwa ngazi tano
ikiwemo kuhifadhi Juzuu 20,10, tano na tatu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)