Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Mashetani
wekundu, Manchester United, rasmi wamefungua njia kwa mshambuliaji wao
Wayne Mark Rooney baada ya kusema hawana mpango wa kukaa chini na nyota
huyo kuhusu kusaini mkataba mpya wa kuichezea klabu hiyo na
wanachohitaji kwa sasa ni kumuangalia uwezo wake uwanjani kabla ya kukaa
mezani kujadili hatima yake Old Trafford.
Mkurugenzi
mkuu wa United Ed Woodward alithibitsha hilo jana wakati klabu yao
ikishuka dimbani katika mchezo wa kwanza tangu waanze ziara yao nchini
Thailand ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu ambapo alisema
kipaumbele kwa sasa nikuangalia dili la uhamisho kama litalipa na sio
kuweka nguvu kubwa ya kukaa na Rooney kujadili hatima yake.
Roonye bado amebakiza miaka miwili katika mkataba wake ambao anakunja kitita cha pauni laki mbili na nusu kwa wiki.
Kwasasa
mshambuliaji huyo amerudi nchini England baada ya kupata majeraha ya
nyama za paja,huku akihusishwa na mpango wa kutimkia konako Chelsea au
kwa matajiri wa Ufaransa , Paris St-Germain, lakini imeshaelezwa na
United kuwa nyota huyo baba wa watoto wawili hatauzwa majira haya ya
kiangazi.
Woodward
alisema: ‘Hakuna majadiliano yoyote yaliyofanyika juu ya kuongezwa kwa
mkataba. Sijakaa na mchezaji yeyote kujadili kuongeza mkataba wake na
hakuna chochote kwenye kitabu changu cha kumbukumbu”
‘Tunaweza kuongopa kuvunjika kwa mkataba na Mchezaji? kiukweli hapana”. Rooney
hakuwepo katika kikosi cha jana cha David Moyes ambapo aliiongoza
United katika mechi ya kwanza dhidi ya Singha All-Stars mjini Bangkok na
kupoteza kwa kufungwa bao 1-0.
Kauli
hii ya kibosile huyo wa United imeongeza nguvu kwa kocha wa Chelsea,
Jose Mourinho ambaye alisema yupo tayari kumwaga kitita cha pauni
milioni 60 ili kumnasa Rooney, lakini naye Laurent Blanc wa PSG amekodoa
macho yake kwa nyota huyo.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)