Pages

LIVERPOOL YASEMA KWA OFA YA PAUNDI MILIONI 50 WAPO TAYARI KUMUACHIA SUAREZ, ARSENAL WAGOMA KUPANDISHA DAU SASA MADRID KUANZA KUMNYEMELEA SUAREZ


Klabu ya Liverpool imekubali kwamba inaweza kuumuza mshambuliaji wa kiuruguay Luis Suarez endapo tu timu inayomtaka italipa kiasi cha paundi millioni 50 - ambayo ndio thamani ya mshambuliaji huyo kwa mujibu wa Liverpool wenyewe.

Juzi usiku klabu ya Arsenal ilivunja bank na kuamua kutoa ofa ya £40million kwa Liverpool kwa ajili ya kumsaini Luis Suarez lakini majogoo wa jiji wakaipiga chini ofa hiyo na kusisitiza kwamba ikiwa Arsenal wanahitaji saini ya Suarez basi inabidi walipe fedha ambayo ni thamani ya kweli ya mshambuliaji ambayo inatajwa kuwa £50m - kwa mujibu wa kocha wa Liverpool Brendan Rogers.

"Ikiwa Arsenal wanamtaka Suarez, then inabidi walipe fedha ambayo inaendana na thamani ya kweli ya mchezaji."

Lakini huku Rogers akisema hivyo imeripotiwa kwamba Arsenal wanataka mshambuliaji mwenyewe alazimishe kuondoka na kujiunga nao.

Arsenal wanaamini kwamba Suarez ameshaamua kwa dhati kuondoka Anfield ili ajiunge na timu inayocheza soka la ligi ya mabingwa wa ulaya.

Na wanaamini ofa yao ya £40m imefikia fedha ambayo inatakiwa kuvunja mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 - kitu ambacho kinawapa ruhusa ya kuongea na mchezaji huyo.

Lakini tatizo kubwa kwa Arsenal ni kwamba wanaamini mshambuliaji huyo angependelea zaidi kujiunga na Real Madrid ambayo nayo imeomnyesha nia ya kumhitaji. 

Real Madrid jana walimuuza mshambuliaji wao Gonzalo Higuain kwenda Napoli kwa ada ya uhamisho wa £32 +nyongeza, na hivyo wanaweza kuja kumalizana na Liverpool muda wowote ikiwa wataachana na mpango wa kumsajili Gareth Bale ambaye anaweza kuwagharimu kiasi kisichopungua £70m.
 
CHANZO: SHAFIH DAUDA BLOG

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)