HATIMAYE STEVAN JOVETIC ATUA RASMI KWA MAN CITY TAYARI KUUNGANA NA ALVARO NEGREDO KUONGOZA MASHAMBULIZI MSIMU UJAO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

demo-image

HATIMAYE STEVAN JOVETIC ATUA RASMI KWA MAN CITY TAYARI KUUNGANA NA ALVARO NEGREDO KUONGOZA MASHAMBULIZI MSIMU UJAO

.com/blogger_img_proxy/Kipaji cha kweli: Kufika kwa  Stevan Jovetic kutaongeza makali ya safu ya ushambuliaji ya Manchester City 
.com/blogger_img_proxy/Uhamisho umekamilika: Alvaro Negredo amesainishwa na City na kupewa jezi namba tisa
.com/blogger_img_proxy/
.com/blogger_img_proxy/
Karibu Manchester: Mshambuliaji raia wa Montenegrin, Jovetic akiwasili katika Hoteli ya Manchester jana usiku
.com/blogger_img_proxy/Mchezaji mwingine mpya kutoka Sevilla, Alvaro Negredo aliingia katika hoteli hiyo usiku wa jana 
.com/blogger_img_proxy/Mwaga wino hapa: Negredo akiwa na mkurugenzi wa michezo wa City , Txiki Begiristain (kushoto) na wakala wake  wakati wa kusaini mkataba  
.com/blogger_img_proxy/
Haina noma, barida tu!:  Nyota huyo atapambana kutafuta namba pamoja na Negredo, Sergio Aguero na  Edin Dzeko 
.com/blogger_img_proxy/
Tayari ametulia zake:  Jovetic amewasili katika klabu mpya ya City na sasa kilichobaki ni kushindana kupata nafasi kikosi cha kwanza
 
Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com

“Negredo, Sergio Aguero na  Edin Dzeko ,Stevan Jovetic”. Washambuliaji hao wote wana viwango vya juu, sasa swali ni moja, nani kuwa chaguo namba moja kwa kocha mpya wa City, Manuel Pellegrini?.

Miamba ya soka nchini England na wenye jeuri ya pesa, klabu ya Manchester City imethibitisha kumsaini mshambuliaji hatari Stevan Jovetic kutoka Fiorentina kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 25.8 baada ya mwanandinga huyo wa kimataifa wa Montenegro kufuzu vipimo vya afya katika dimba maridhawa la Etihad. 

Inaeleweka kuwa City watalipa kiasi cha Pauni Milioni 22.4 na ada itapanda kutokana na kukua kwa malipo ya posho ya nyota huyo mwenye uwezo mkubwa wa kucheka na nyavu. Pia Uhamisho wa nyota mwingine ,  Alvaro Negredo  umethibitishwa, huku  akikabidhiwa  jezi namba tisa.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Pages