Mkuu wa Majeshi Jenerali Mwamunyange
--
Katika siku za karibuni kumekuwa na kauli kadhaa kutoka kwa baadhi ya viongozi wa nchi jirani ambazo zinatafsiriwa na wananchi kwamba ni za kuitisha Tanzania.
Katika siku za karibuni kumekuwa na kauli kadhaa kutoka kwa baadhi ya viongozi wa nchi jirani ambazo zinatafsiriwa na wananchi kwamba ni za kuitisha Tanzania.
Jenerali Mwamunyange alisema jeshi wakati wote
liko imara kuwalinda wananchi na nchi kwa jumla hivyo
wasiogope...“Endeleeni na shughuli zenu na msiogope mtu yeyote, fanyeni
kazi zenu bila wasiwasi.”
Huku akishangiliwa na mamia ya watu waliohudhuria
maadhimisho hayo, Jenerali Mwamnyanye alisema yeyote atakayethubutu
kuchezea usalama wa nchi atakiona cha mtema kuni.Akizungumzia Siku ya Mashujaa, Rais Kikwete
alisema ni siku ya kuwakumbuka mashujaa waliojitolea maisha yao wakati
wa Vita ya Kagera kuilinda nchi yao ili iwe salama na yenye amani.
“Kuhakikisha usalama wa nchi kuna gharama yake
kwani kuna wengine walikufa na wengine wakabaki na vilema kwa ajili ya
hilo.Wale ambao wamebaki na wana matatizo lazima tuwaangalie vizuri na
vile ambavyo havijafanyika tutavishughulikia kwani kutetea taifa ni kazi
ngumu.”
Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na
viongozi
mbalimbali wakiwamo, Makamu wa Rais, Dk Gharib Bilal,Rais wa Zanzibar,Dk
Mohammed Shein, Jaji Mkuu wa Tanzania,Othman Chande na Jaji Mkuu wa
Zanzibar,Omar Othman Makungu ambao wote walipewa nafasi ya kuwasalimia
wananchi waliohudhuria maadhimisho hayo.
Kwa Habari Zaidi Bofya na Endelea.......
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)