CHRISTIAN BENITEZ AFARIKI DUNIA AKIWA NA MIAKA 27 TU, MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALA PEMA PEPONI, AMINA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

CHRISTIAN BENITEZ AFARIKI DUNIA AKIWA NA MIAKA 27 TU, MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALA PEMA PEPONI, AMINA

Tragic: Christian Benitez, in action for Birmingham, has died aged 27 after suffering a heart attack
Tanzia: Christian Benitez, aliyekuwa anaichezea Birmingham, amafariki dunia akiwa na miaka 27 kwa matatizo ya shinikizo la damu Shirikisho la soka la Ecuador limetoa taarifa kuwa: “FEF inasikitika kutangaza kifo cha Christian Benitez, mshambuliaji wa  klabu ya  Qatar ,  Al Jaish na timu ya taifa ya  Ecuador “.

‘Benitez, alikuwa na klabu yake mpya nchini Qatar, baada ya mchezo alikumbwa na maumivu makali ya tumbo na kupelekwa hospitali na saa chache baadaye alipoteza maisha” Shirikisho hilo limetoa pole kwa familia ya marehemu Benitez, wazazi, mke, watoto, ndugu, jamaa na marafiki wa Christian Benetiz. Mwenyezi Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya marehemu. Amen
National star: Benitez (right) won 58 caps for Ecuador, including this World Cup Qualifier against Peru last monthNyota Benitez (kulia)  enzi za uhai wake 
Tribute: Manchester United winger Antonio Valencia (left) posted this photo of him and friend BenitezMungu ampumzishe mahala pema peponi: Winga wa Manchester United ,  Antonio Valencia (kushoto) akiwa katika pozi na rafiki yake  Benitez enzi za uhai wa marehemu.

Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
“Kifo hakina Huruma” alishaimba Doctor Remy Ongala aliyetangulia mbele ya haki, Matonya aliimba Dunia Mapito, tuombeana wote ili tuende salama, kwani hujui siku yako lini”, pia Kila nafsi itaonja mauti. Lakini inauma sana unapompoteza ndugu ndani ya muda mfupi angali bado unamhitaji.

Safari ya CHUCHO hapa Duniani yakamilika akiwa kijana mdogo. Mchezaji Christian Benitez, Chucho, aliyekuwa anaichezea klabu ya  Birmingham City nchini England ambaye kwa sasa alikuwa anaichezea klabu ya El Jaish ya Qatary, amefariki dunia akiwa na miaka 27 kwa matatizo ya shinikizo la damu.

Nyota huyo raia wa Ecuador aliyekuwa anawaniwa na Tottenham majira haya ya joto alikamilisha dili la uhamisho la pauni milioni 10 na kuelekea El Jaish akitokea katika klabu moja ya Mexco wiki chache zilizopita. Benitez aliichezea timu yake jana usiku dhidi ya Qatar SC, lakini dakika chache baada ya mechi alilazwa hospitalini kwa matatizo ya maumivu makali ya tumbo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages