Mfunguzi: Mchezaji anayefanya majaribio katika klabu ya Chelsea Bertrand Traore (katikati) akiandika kimiani bao la kwanza
Romelu Lukaku akipachika kambani bao lake
Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Chelsea
imeendeleza rekodi ya ushindi katika ziara yake barani Asia baada ya
kuwafunga mabao 4-1 mastaa wote wa ligi ya Malaysia dimba la Shah Alam
, lakini hali imekuwa mbaya kwa kocha Jose Mourinho baada ya kuumia kwa
nyota wake Kevin de Bruyne. De Bruyne alitolewa uwanjani kwa machela baada ya kuumia goti lake wakati akitia kambani bao la pili kwa klabu yake.
Mabao
ya Chelsea yalitiwa kambani na Traore (dakika ya 5), De Bruyne ( dakika
ya 28), Lukaku (dakika ya 45+4), Moses (dakika ya 88). Alipoulizwa
kuhusiana na majeruhi ya nyota huyo raia wa Ubelgiji, bosi wa Chelsea
Jose Mourinho alisema: ‘Wakati akiwa amelala chini na kuomba kufanyiwa
mabadiliko, kila mtu katika benchi letu alijisikia vibaya sana”.
Mourinho
alisisitiza kuwa katika mechii hiyo, Bruyne ameonesha kiwango cha juu
na kumshawishi kila mtu, na hii inaonesha atakuwa mchezaji muhimu katika
kikosi chake.
Lakini uchunguzi wa awali haujaonesha kama tatizo ni kubwa sana, hivyo ni matarajio kuwa nyota huyo atarudi mapema uwanjani.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)