Pages

CESC FABREGAS AONGEZEWA DAU HADI KUFIKIA PAUNI MILIONI 30 NA BOSI MPYA WA MAN UNITED DAVID MOYES KWAAJILI YA KUICHEZEA MAN U MSIMU UJAO

Cesc Fabregas akiwa ndani ya uwanja msimu uliopita

Hatimaye katika kusaka kile kilicho bora Bosi Mpya wa Manchester United David Moyes amesema yupo tayari kuongeza Dau kwa Mchezaji wa Zamani wa Arsenal ambaye Sasa anakipiga katika klabu ya Barcelona iliyopo Nchini Hispania kwaajili ya Kuimarisha Kikosi Chake katika Msimu ujao wa Ligi kuu ya Uingereza na ligi mbalimbali za kimataifa Pamoja na Bosi huyo Mpya wa Manchester United David Moyes kutangaza kuongeza Dau hili hadi kufikia Paundi Milioni 30 Klabu hiyo ya Hispania imetoa angalizo kwa Mabingwa hao wa Ligi kuu ya Uingereza Kuwa hawapo tayari kumuuza Mchezaji huyo wa Zamani wa Arsenal ambaye alijiunga na Mabingwa hao wa Hispania mwaka 2011.

Makamu wa Raisi wa Klabu hiyo iliyopo katika Dimba la Nou camp Nchini Hispania Josep Maria Bartomeu alikaririwa na Gazeti la Kila la Michezo la Hispania akisema kuwa "Barcelona inawahakikishia kuwa hatupo tayari kwaajili ya kumruhusu Cesc Kuondoka Barcelona na Cesc hauzwi"

Hapo awali Bosi huyo wa Manchester United David Moyes alipeleka dau la Pauni milioni 25 wiki iliyopita ambapo alishindwa kwa kumshawishi Kiungo huyo wa Zamani wa Arsenal Cesc Fabregas kujiunga na Manchester United Siku Chache baadae ndipo Bosi huyo aliyemrithi Kocha Sir Alex Ferguson Kuja na Dau jipya la Pauni Milioni 30 kwa Kiungo huyo wa Barcelona aliyejiunga Mwaka 2011 akitokea kwenye Klabu ya Arsenal ya jijini London.

Endapo atafanikiwa kumnyaka kiungo huyo wa Zamani wa Arsenal na Mchezaji wa Barcelona Kwa ada ya Pauni Milioni 30 Basi kwa mara ya Kwanza David Moyes atakuwa ametoa Dau kubwa katika Usajili wa Msimu huu na ndio litakuwa dau lake la Kwanza kubwa kwaajili ya Kumnasa kiungo huyo wa Barcelona

Naye Mlinda Mlango namba moja wa Manchester United David Gea amesema anamkaribisha Kiungo huyo wa Barcelona Cesc Fabregas kuungana na Mabingwa hao wa Uingereza. David Gea alikaririwa na Daily Mail akisema kuwa " Ni Mchezaji Mkubwa, mwenye ujuzi wa hali ya juu,ambaye anajua kushinda mambo na siku zote ndio mchezaji anayehitaji kwa klabu.

Robin Van Persie naye ameonyesha kutaka Cesc kuungana na Mabingwa hao wa Uingereza na kuboresha nafasi ya viungo katika kikosi hiko cha Mashetani wekundu.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)