Omari Kimweri |
BONDIA Mtanzania Omari Kimweri 'Lion
Boy 'anaefanya shughuli zake nchini Australia amendelea kutamba katika
nchi hiyo baada ya jana kumtwanga kwa KO ya raundi ya kwanza bondia Ekkalak Saenchan wa Thailand ikiwa ni mchezo wake wa 16 tangia angie katika ngumi za kulipwa akiwa nchini humo
Bondia huyo ambaye anaitangaza vema
nchi ya Tanzania Kimataifa ameaidi kuwa ataenderea kutoa vipigo kwa
mabondia mbalimbali pindi wakutanapo ulingoni
Bondia huyo aliezaliwa Tanzania katika jiji la Dar es salaam mwaka
1982 amekuwa gumzo nchini humo kwa kuonesha mchezo mzuri unaowavutia
raia wengi wa Australia na kuweza kuwa bondia namba moja katika nchi
hiyo uku katika Dunia akishikilia nafasi ya 52 katika mabondia 450
duniani wenye uzito wa light flyweight
Anasema lengo lake kubwa ni kuukamata
ubingwa unaotambulika kimataifa Duniani wa WBA World light flyweight
title unaoshikiliwa na bingwa namba moja Duniani ,Roman
Gonzalez na IBF light flyweight title unaoshikiliwa na
John Riel
Casimero wa Philippines ambao wananiumiza kichwa kwa sasa kwani ngumi ulimwengu mzima ni zile zile ila tunazidiana maarifa
Bondia huyo anaefanya shughuli zake za
masumbwi nchini Australia ana mpango wa kuja kuwekeza nchini Tanzania
mchezo wa masumbwi ili ukuwe hapa ambapo atafanya kila jitiadi ili
mchezo wa masumbwi uweze kusonga mbele nchini habari hizi kwa
ushirikiano mkubwa wa mtandao wa www.superdboxingcoach. blogspot.com
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)