Pages

Basi la abiria laungua moto

ZAIDI ya Abiria hamsini wamenusurika baada ya Basi walilokuwa wakisafiria kuungua moto wakati wakielekea Mkoani Mwanza.

Kamanda wa polisi Mkoani Tabora,Kamishna msaidizi wa Polisi,Peter Ouma,amesema tukio hilo limetokea eneo la Nata mjini Nzega juzi usiku majira ya saa mbili likihusisha basi la Princess Muro lenye namba za usajili T 979  CBH.

Amesema wakati basi hilo lililokuwa likitokea Dar.es.salaam kwenda mwanza likiendeshwa na Boniface francis lilipata hitilafu kwenye Injini na kuanza kuwaka moto.

Kamanda ouma amesema bahati nzuri abiria walitahadharishwa kushuka kabla madhara hayajawa makubwa n ndio maana hakuna abiria aliyejeruhiwa isipokuwa baadhi ya mizigo ndio imeungua.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)