ZAIDI ya
Abiria hamsini wamenusurika baada ya Basi walilokuwa wakisafiria kuungua moto
wakati wakielekea Mkoani Mwanza.
Kamanda
wa polisi Mkoani Tabora,Kamishna msaidizi wa Polisi,Peter Ouma,amesema tukio
hilo limetokea eneo la Nata mjini Nzega juzi usiku majira ya saa mbili
likihusisha basi la Princess Muro lenye namba za usajili T 979 CBH.
Amesema
wakati basi hilo lililokuwa likitokea Dar.es.salaam kwenda mwanza likiendeshwa
na Boniface francis lilipata hitilafu kwenye Injini na kuanza kuwaka moto.
Kamanda
ouma amesema bahati nzuri abiria walitahadharishwa kushuka kabla madhara
hayajawa makubwa n ndio maana hakuna abiria aliyejeruhiwa isipokuwa baadhi ya
mizigo ndio imeungua.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)