UONGOZI wa kampuni ya Bakhresa inayomiliki klabu ya Azam umemwaga dola milioni moja (zaidi ya Sh bilioni 1.6) ili kupata haki ya udhamini wa Ligi Kuu Bara kama warushaji wa matangazo ya televisheni.

Kutokana na kumwaga fedha hizo, kampuni hiyo kupitia kituo chake kipya cha televisheni yake ya Azam TV, kitakachoanza kurusha matangazo hivi karibuni, kitapewa haki ya kuonyesha mechi zote za Ligi Kuu Bara. Kampuni hiyo iliyokuwa inapambana na Supersport ya Afrika Kusini iliyokuwa tayari kutoa dola 500,000 imeihakikishia bodi ya ligi hiyo kuwa iko tayari kutoa fedha hizo na kila klabu zikiwemo Yanga na Simba zitapata Sh milioni 140 kila moja kwa msimu. Pamoja na fedha hizo kutoka kwa wamiliki hao wa Azam FC ambayo ndiyo wapinzani wakubwa wa Simba na Yanga, klabu hizo kongwe zimesema zinataka kulipwa zaidi kwa kuwa ndiyo zenye mashabiki wengi.
Katika kikao kilichofanyika juzi, kumezuka mjadala mkubwa huku Simba na Yanga zikisisitiza kwamba haitakuwa haki zenyewe kupewa Sh milioni 140 sawa na klabu nyingine ambazo zina mtaji mdogo wa mashabiki. “Lakini watu wa bodi ya ligi wameonyesha kutokuwa waungwana maana wameendelea kulazimisha Simba na Yanga zilipwe sawa na klabu hizo ndogo. Sisi tunaona hii si sahihi,” kilieleza chanzo cha uhakika.
SOURCE:GLOBAL PUBLISHER BLOG
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)