Airtel, UNESCO wazindua mradi wa kuwawezesha radio za kijamii nchini - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Airtel, UNESCO wazindua mradi wa kuwawezesha radio za kijamii nchini


Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Masawe akisalimiana na baadhi ya watoto wa mtandao wa wanahabari alipowasili kwenye uzinduzi wa kurusha matangazo ya Redio FADECO kwenye mnara wa Airtel wilayani Karagwe mkoani Kagera, kulia kwake ni Meneja Mahusiano ya Jamii wa Airtel Tanzania Hawa Bayumi.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Masawe akijianda kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mradi huo, anayeshuhudia tukio hilo ni Meneja Mahusiano ya Jamii wa Airtel Tanzania Hawa Bayumi na wa kwanza kulia ni Meneja wa Biashara wa Kanda wa Airtel Ally Maswanya.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Masawe akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Redio ya kijamii ya Wilayani Karagwe ya FADECO Joseph Sekiku (katikati) wakati hafla ya uzinduzi huo. Kushoto ni Meneja Mahusiano ya Jamii wa Airtel Tanzania Hawa Bayumi.
Mkurugenzi wa Redio ya kijamii ya Wilayani Karagwe ya FADECO Joseph Sekiku (wa kwanza ) akitoa maelezo juu ya kituo cha radio kwa Mipango Taifa Kitengo cha Mawasiliano na Habari UNESCO Yusuph Al Amin alipotembelea Studio za Redio hiyo inayorusha matangazo kwa ushirikiano wa Airtel na UNESCO wakati wa uzinduzi wa ushirikiano huyo uliofanyika Karagwe Bukoba .
Meneja wa Kituo cha redio ya Jamii FADECO Adelina Lwedamula akitoa maelezo machache ya utengenezaji wa vipindi kwa Meneja Mahusiano ya Jamii wa Airtel Tanzania Hawa Bayumi alipotembelea Studio za Redio hiyo inayorusha matangazo kwa ushirikiano wa Airtel na UNESCO wakati wa uzinduzi wa ushirikiano huyo uliofanyika Karagwe Bukoba .

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages