MSANII
wa nyimbo za asali za utamaduni wa Kigogo ambaye anatamba ndani na nje
ya Tanzania, Msafiri Zawose, anatarajia kupiga shoo ya aina yake maalum
ya kuchangia kituo cha AMAP Juni 28, katika mgahawa wa PoaPoa uliopo
mjini hapa.
Akizungumza
jana Zawose ambaye ni mtoto wa marehemu Hukwe Zawose aliyerithi
kipaji cha baba yake kwa kuendeleza utamaduni wa kabila hilo la Wagogo,
alisema maandalizi ya shoo hiyo yamekamilika na tayari tiketi zimeanza
kuuzwa.
"Wadau
wajitokeze kwa wingi kwenye shoo yetu maalum ya kusaidia kituo cha
AMAP kwa ajiri ya kuwasaidi watoto wasio jiweza kulipa ada zao za shule"
alisema Zawose.
Na
kuongeza kuwa mbali na burudani ya muziki pia kutakua na maonesho ya
bidhaa mbalimbali sambamba na chakula cha tanzania kilichochanganya na
usasa.
"Nyimbo ni kama asili yangu, kuna vibao kama Ilima, Mahera na vingine vingi"alimalizia Zawose.
kubainisha kuwa, burudani hiyo itatolewa na yeyey kwa pamoja na bendi yake hiyo ya Sauti Band.
Kwa
upande wake Hannah Nelson wa walioandaa shoo hiyo alisema tiketi
zinapatikana katika mgahawa huo wa Poa Poa kwa bei tsh 15,000, huku
siku ya tukio Juni 28, mlangoni itakuwa tsh 20,000 ambapo kiingilio
hicho kinajumuisha na chakula.
"Tiketi zinapatikana Poa Poa Restaurant, karibiuni sana katika shoo hii ambayo ni maalum kuchangia elimu" alisema Annah.
Shoo hiyo inatarajia kuanza majira ya saa 12 jioni hadi saa Sita usiku.
Kituo
hicho cha AMAP (Africa Modern Art Project) kinajishughulisha na
shughuli za sanaa mjini hapa na pia kinasomesha watoto wadogo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)