TGNP yakabidhi Vifaa vya Mawasiliano Vituo vya Taarifa na Maarifa - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TGNP yakabidhi Vifaa vya Mawasiliano Vituo vya Taarifa na Maarifa

Ofisa katika Kitengo cha Habari na Mawasiliano TGNP, Deogratius Temba, akikabidhi vifaa hivyo kwa wanakituo hicho.

MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP),  umepanua wigo wa mawasiliano kwa makundi ya pembezoni hasa wanwake kwa kuwapatia vifaa vya teknolojia ya habari na Mawasiano (TEHAMA) kwaajili ya kupashana habari katika Kituo cha taarifa na maarifa Mkambarani Morogoro Vijijini.

Akikabidhi vifaa hivyo vyenye dhamani ya zaidi ya shilingi Milioni 1.9, Ofisa katika Kitengo cha Habari na Mawasiliano TGNP, Deogratius Temba, amesema kuwa  shirika hilo limeamua kutoa vifaa hivyo kwaajili ya kuhakikisha makundi yaliyoko pembezoni hasa wanawake wanafikiwa kwa kupata taairfa sahihi kwa wakati muafaka na kuwawezesha pia wao kutoa taraifa walizo nazo katika ngazi ya jamii.

“Huu ni mradi unaowezesha sauti za jamii kusikika,  kuanzishwa kwa ‘Sauti ya Jamii’ kunawezesha  sauti za wanawake wengi kupewa taarifa na kutoa na kusikika, Tunajua hii itawezesha wanawake wengi  kupaaza sauti zao na kupambana na matukio ya ukatili wa kijinsia pamoja na changamoto nyingine zilizoibuliwa wakati wa Utafiti raghibishi mwaka 2012 na tamasha la Jinsia la mwaka 2012 hapa Mkambatani” alisema Temba

Alisema kuwa TGNP kwa muda mrefu imekuwa ikitumia TEHAMA kwa ajili ya mawasiliano, kuwafikia wadau mbalimbali, kujenga nguvu za pamoja   katika kuleta mabadiliko chanya.  Matumizi ya ujumbe mfupi wa simu  (SMS) imekuwa ni  moja ya TEHAMA ambayo  inatumika kwa wingi katika ngazi ya jamii. 

“Kwa mantiki hii TGNP imeona fursa kubwa ya kutumia ujumbe mfupi  kama nyenzo ya  kusaidia kuunganisha nguvu katika kuhabarishana na kuchukua hatua za kwajibisha  mamlaka na kuleta mabadiliko chanya” aliongeza.
Sauti ya jamii itatumia  teknolojia  ya bulk SMS yaani kutuma ujumbe  mfupi wa simu kwa kutumia computer kwa watu wengi zaidi ya 10,000 kwa wakati mmoja.  Sauti ya jamii  itasaidia  kupashana habari  kupitia kituo cha taarifa na maarifa cha jamii kwenda wa wadau mbali mbali wakiwemo wanaharakati waliohusika katika Utafiti wa mwaka jana, madiwani,  Wanajamii wa Mkambarani, kamati mbalimbali  za maendeleo Mkambarani,  viongozi wa serikali za mtaa , kata hadi wilaya, madiwani na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali.   

Makamu Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Mkambarani, Teresia Berege, alisema kuwa kuwepo kwa Kituo hicho na vifaa hivyo vya kisasa kutasaidia  kurahisisha mawasiliano, upashanaji wa taarifa na kupata habari kwa haraka itakuwa ni ukombozi kwa watoto na wanawake na kuwaweka katika mazingira bora ya kupata maendeleo.

Naye Diwani wa kata ya Mkambarani, danile Shawa alisema kuwa wanaharakati wa Mkambarani wanapaswa kutumia vizuri vifaa vilivyotolewa na TGNP ili vilete ufanisi na maendeleo kwa wakazi wa kata hiyo.

“ninawashauri mtumie vema hivi vitu, kwa hapa kwetu Mkambarani hii ni fursa ya pekee, tumepiga hatua sasa, tekonoljia ilikuwa nyuma sasa TGNP imewawezesha mnakwenda na wakati, mtumie vizuri kwa uaminifu na unagalifu na msitume taarifa ambazo hazina ukweli” alisema Diwani.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages