Moto ukiwaka katikati ya barabara wakati wa vurugu zilizotokea katika viwanja vya SOWETO mjini Arusha.
Baadhi ya
watu wakifunga barabara baada ya kutawanywa na Polisi kwa mabomu ya
machozi katika viwanja vya SOWETO vilivyopo jijini hapa, Barabara Kuu
inayopitisha magari ya mikoani eneo la Kimahama
Moto uliowashwa na baadhi ya watu
wakifunga barabara baada ya kutawanywa na Polisi kwa mabomu ya machozi
katika viwanja vya SOWETO vilivyopo jijini hapa, barabara Iiliyopo eneo
la Kaloleni.
Sehemu
ya Umati na wananchama na mashabiki wa chadema waliyojitokeza viwanja
vya soweto mjini arusha kuaga miili ya watu walifariki dunia kutokana na
mlipuko wa bomu uliyotokea mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye mkutano
wa chadema
Mnadhimu
mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni na mbunge wa singida
mashariki-chadema Tundu lissu akihutubia sehemu ya mamia na wapenzi wa
chadema waliyojitokeza viwanja vya soweto mjini arusha kuaga miili ya
watu
walifariki dunia kutokana na mlipuko wa bomu uliyotokea mwishoni mwa
wiki iliyopita kwenye mkutano wa chadema
Wanafunzi
wa shule wakijiziba na nguo na kunawa uso baada ya kudhuriwa na mabomu
ya machozi yaliyopigwa leo na Polisi waliokuwa wakitawanya maelfu ya watu waliokuwa kwenye mkutano katika viwanja vya SOWETO.
Askari
wa jeshi la polisi wakilinda uwanja wa soweto mjini arusha muda mfupi
baada ya kuwatawanya mamia ya wafuasi wa chadema waliyojitokeza
waliyojitokeza viwanja vya soweto mjini arusha kuaga miili ya watu
walifariki dunia kutokana na mlipuko wa bomu uliyotokea mwishoni mwa
wiki iliyopita kwenye mkutano wa chadema.Picha zote na Ferdinand Shayo
---
Jeshi la polisi mkoani
Arusha linawashikilia viongozi wanne wa CHADEMA na watu wengine 60 huku
likiendelea kuwatafuta wabunge wawili wa chama hicho na watu wengine.
Kamishina wa Operesheni wa Mafunzo wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Paul Chagonja amesema licha ya watu hao kukamatwa pia wamekamata pikipiki 106 na baiskeli 16 ambazo zilitelekezwa.
Chagonja amewataja wanne hao waliotiwa nguvuni kuwa ni Tundu Lissu (Singida Mashariki), Mustapha Akonay (Mbulu) Said Arfi (Mpanda Mjini) na Joyce Nkya (Viti Maalumu).
Kamishina wa Operesheni wa Mafunzo wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Paul Chagonja amesema licha ya watu hao kukamatwa pia wamekamata pikipiki 106 na baiskeli 16 ambazo zilitelekezwa.
Chagonja amewataja wanne hao waliotiwa nguvuni kuwa ni Tundu Lissu (Singida Mashariki), Mustapha Akonay (Mbulu) Said Arfi (Mpanda Mjini) na Joyce Nkya (Viti Maalumu).
Chagonja
amesema limewatia nguvuni watu hao kwa makosa ya kuhutubia mkutano
haramu wakati wa kuwaaga marehemu waliopoteza maisha kwenye mlipuko wa
bomu uliotokea katika viwanja vya Soweto (al maarufu viwanja vya AICC)
jijini humo mwishoni mwa wiki.
- Taarifa iliyonukuliwa kutoka kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, inasema kuwa uchunguzi wa haraka umebaini kuwa bomu lililotumika kulipua katika mkutano huo wa CHADEMA hivi majuzi limetengezwa nchini China, na aina hiyo ya mabomu yanamilikiwa na vyombo vya dola, hasa Jeshi la Wananchi (JWTZ).
Amesema wataendelea kubaki korokoroni hadi uchunguzi utakapokamilika.
Wanaotafutwa ni pamoja na Mwenyekiti CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ambao waliponyoka mikono ya polisi.
Wabunge wengine wanaotajwa kuwepo uwanjani hapo ni pamoja na John Mnyika na Ezekiah Wenje.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)