Msanii
wa Filam, nchini, Jaqueline Wolper, akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu Tamasha hilo, wakati wa mkutano huo uliofanyika jijini Dar es
Salaam
Meneja
Habari na Mawasiliano wa TBL, Edith Mushi (katikati) akizungumza na
waandishi wa habari, wakati wa mkutano huo (kushoto) ni Mkurugenzi wa Sophia Records walio waandaaji na waasisi wa tamasha hilo, Musa Kissoky.
**************************************
Na Mwandishi Wetu
TAMASHA la Wazi la Filamu Tanzania maarufu kama ‘Grand Malt Tanzania Open
Film Festival’ mwaka huu linatarajiwa kufanyika katika Viwanja vya Sahara
jijini Mwanza.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa tamasha hilo uliofanyika jijini Dar
es Salaam jana, Meneja wa kinywaji cha Grand Malt, Consolata Adam alisema, wanaamini
litafanikiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na mikakati waliyoiweka.
Consolata alisema, tamasha hilo linatarajiwa kufanyika katika viwanja hivyo
kuanzia Julai 1-7, mwaka huu huku kukiwa na filamu mbalimbali zitakazoonyeshwa
katika kipindi hicho.
“Tumejipanga kufanya uhamasishaji wa kutosha ili
kuwawezesha wakazi wa Mwanza na maeneo ya jirani kuweza kuhudhuria tamasha
hili. Tunawakaribisha watu wote wenye mapenzi na filamu zetu za Tanzania kufika
na kushuhudia tamasha hili ambalo mwaka huu limeboreshwa zaidi,” alisema Consolata.
Naye Meneja Habari na Mawasiliano wa TBL, Edith Mushi alisema kwa
ushirikiano na kampuni ya Sophia Records, ambao ndio waandaaji na waasisi wa
tamasha hilo, wanaamini litafana na kufanikiwa zaidi mwaka huu.
“Tumeona jinsi wananchi wanavyozipenda filamu za Tanzania maarufu kama
‘Bongo Movies’ na jinsi walivyo na kiu ya kuwaona wasanii wa filamu ana kwa ana,”
alisema.
Edith alisema waliingia mkataba wa miaka mitatu wa kudhamini tamasha hilo
na kwa sasa wanalipeleka mikoa mingine kama walivyofanya kwa kulipeleka Mwanza
kutoka Tanga lilikofanyika mwaka jana.
“Tunawaahidi Watanzania wote kwa ujumla, kuwa tamasha hili litakuwa na
mvuto wa aina yake na hatimae kutumika kulitangaza Taifa letu kupitia tasnia
hii ya filamu ambayo kwa sasa inakua kwa kasi kubwa,” alisema Edith na kutaka
kampuni au taasisi nyingine kujitokeza ili kuwa wadhamini wenza.
Naye Mkurugenzi wa Sophia Records walio waandaaji na waasisi wa tamasha
hilo, Musa Kissoky alitoa shukrani kwa Grand Malt kulidhamini hivyo kuliboresha
kwa kiasi kikubwa.
“Tunawashukuru sana Grand Malt na wasanii wa Bongo Movie, hususan uongozi
wao, kwa ushirikiana mkubwa wanaotupatia katika kuhakikisha tamasha hili
linafanikiwa.”
Tamasha hilo litakuwa likianza asubuhi hadi usiku na kutakuwepo na
burudaniu mbalimbali zitakazosindikiza na hakutakuwa na kiingilio, huku akisema
bendi ya Extra Bongo watakuwepo siku ya uzinduzi.
Wasanii wote maarufu wa filamu wanatarajia kutua Mwanza Juni 29, ambapo
siku hiyo watajumuika na wakazi wa Mwanza ndani ya Club Lips na siku inayofuata
watashiriki katika shughuli za kijamii katika hospitali ya Mkoa wa Mwanza ya
Sekou Toure, ambapo watatoa vyandarua zaidi ya 1000.
Akizungumzia tamasha hilo, mwigizaji Jacqueline Wiolper alisema, wana
furaha kubwa na wanaamini watapata mengi zaidi wakati wote wa tamasha hilo.
Tamasha hilo linadhaminiwa kwa mwaka wa tatu sasa na kinywaji kisicho na
kilevi cha Grand Malt kinachozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)