Mshambuliaji wa Sifa United Haruna Athuman (kushoto) akichuana na Alex
Simenga wa Mtakuja Beach wakati wa mechi ya vijana chini ya umri wa
miaka 17 ya Airtel Rising Stars, mkoa wa Kinondoni, iliyochezwa kwenye
uwanja wa Mwanamanyala Shule ya Msingi jijini Dar es Salaam leo Juni 24,
2013. Sifa United walishinda 5-2.
Alphonce Shabani wa Mtakuja Beach (kulia) akimtoka Haruna Athuman waf
Sifa United wakati wa mechi ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya
Airtel Rising Stars, mkoa wa Kinondoni, iliyochezwa kwenye uwanja wa
Mwanamanyala Shule ya Msingi jijini Dar es Salaam leo Juni 24, 2013.
Sifa United walishinda 5-2.
Abdulazizi Haruna wa Mtakuja Beach na Hamir Sheh wa Sifa United
wakiwania mpira wa juu wakati wa mechi ya vijana chini ya umri wa miaka
17 ya Airtel Rising Stars, mkoa wa Kinondoni, iliyochezwa kwenye uwanja
wa Mwanamanyala Shule ya Msingi jijini Dar es Salaam leo Juni 24, 2013.
Sifa United walishinda 5-2.
Baada
ya kubamizwa 3-1 na Makumbusho United siku ya Jumapili Sifa United ya
Manzese jana ilisahihisha makosa yake na kuiadihbu Mtakuja Beach 5-2
katika michuano ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka U-17 ya Airtel
Rising Stars, mkoa wa Kinondoni, kwenye uwanja wa shule ya msingi
Mwananyamala jijini Dar es Salaam.
Sifa
United walianza mashambulizi mara tu baada ya kipyenga cha kwanza na
kufanikiwa kupata goli la kwanza dakika ya tatu kupitia kwa Karim
Athuman aliyeachia shuti kali na kumshinda golikipa wa Mtakuja Beach.
Kabla vumbi halijatulia, Sifa United walifanya shambulio jingine la
nguvu na kufanikiwa kuandika goli la pili mnamo dakika ya sita kupitia
kwa Mustafa Yusuf.
Timu
hiyo ya Manzese uliutawala mchezo katika kila idara na kufanikiwa
kupata goli la tatu dakika ya 25 kupitia kwa Jumbe Evon ambaye aliwatoka
walinzi wa Mtakuja Beach na kuukwamisha mpira wavuni huku akishangiliwa
na washabiki wa timu hiyo. Baada ya hapo, Mtakuja Beach walikuja juu na
kufanikiwa kupata goli dakika ya 39 kupitia kwa Alex Simega. Hadi
mapumuzika magoli yakuwa 3-1.
Baada
ya kutoka mapumuziko, Sifa United waliendelea kulisakama lango la
Mtakuja Beach na juhudi zao zilizaa matunda tena katika dakika ya 53
ambapo mshambuliaji Mustafa Yusuf alifunga goli la nne kabla ya Mtakuja
kufunga goli la pili dakika ya 75 kupitiia kwa Steven Munyu.
Mchezaji
wa Sifa United Mustafa Yusuf ambaye alikuwa nyota wa mchezo huo
alidhihirisha umwamba wake pale alipofunga goli lake la tatu yaani ‘hat
trick’ katika dakika ya 81 baada kugongeana vema na washambuliaji
wenzake. Kufuatia ushindi huo Sifa United kesho Jumanne itapambana tena
na Makumbusho na mshindi wa mchezo huo ndio atakayetawazwa kuwa bingwa
wa ARS mkoa wa Kinondoni 2013.
Programu
hii ya Airtel Rising Stars ni ya Afrika nzima likiwa na lengo la
kuendeleza na kukuza mpira wa miguu katika bara la Afrika kwa vijana
wanaochipukia waweze kupata nafasi ya kuendeleza vipaji vyao.
Fainali
za ARS Taifa vile vile zitatumika kuchagua timu bora za wavulana na
wasichana ambao wataiwakilishaTanzania katika mashindano ya kimataifa
ambapo nchi mwenyeji wa michuano hiyo itatangazwa mwezi ujao. Wachazeaji
wengine watachaguliwa kwenda kwenye kliniki itakayoendeshwa na makocha
kutoka klabu maarufu duniani ya Manchester United
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)