Ulinzi
mkali ambao tayari upo na utazidi kuonekana wakati wa Ujio wa Rais wa
Marekani umewafanya baadhi ya Watanzania kujihisi wanadunishwa au
kuabishwa. Wapo wengine ambao wanaona kuwa hatua mbalimbali za kiusalama
zinazochukuliwa kumlinda Obama, Familia yake na ujumbe wake zinaonesha
dharau na kutoaminiwa kwa vyombo vyetu vya ulinzi. Wengine wanafika
mahali pa kuhisi kuwa Wamarekani wanatudharau sana kiasi kwamba
wanatuchagulia nani aonene na Obama (rejea taarifa kwenye gazeti la
Mwananchi la leo). Watanzania hawapaswi kujisikia hivyo hata kidogo.
Ulinzi wa Obama ni Mkali iwe ndani ya Marekani au Nje
Wakati
wowote Rais wa Marekani anaposafiri iwe ndani ya Marekani au nje ya
Marekani ulinzi wake ni mkali na karibu kamili (almost absolute).
Kuanzia angalia ambalo anakuwepo (linakuwa no fly zone) na kuwa anaenda
na kila kitu kinachoweza kutumika wakati wowote wa dharura yoyote
inayoweza kufikirika kutokea. Kuanzia majanga ya moto, maji, maandamano
ya kisiasa au hata mapinduzi ya kijeshi ulinzi wa Rais wa Marekani
umejiandaa.
Mfano mzuri ni kuwa ikulu ya Rais pale DC – Jumba
Jeupe – juu kabisa kuna mzinga wa kutungua ndege – surface to air
battery. Lakini kubwa zaidi ni kuwa anga lote linalozunguka Ikulu hiyo
ni eneo ambalo ndege haziruhusiwi kuruka (prohibited airspace). Na
wakati wowote Rais anaposafiri mahali popote ndege haziruhusiwi kuruka
juu yake. Anapotua kwenye uwanja kwa mfano hapa Detroit, hakuna ndege
nyingine itakuwa inatua wakati huo huo! Sasa kama hili linatokea
Marekani kwa kiasi gani linaweza kutokea Tanzania?
Ripoti hii
maalum basi ina lengo la kuwasaidia Watanzania kutokwazika na kiasi cha
ulinzi ambao Obama anakuja nao pamoja na usumbufu unaotokana na hilo.
Kama msafara wa Rais Kikwete huwa unazusha usumbufu kwa watu basi wa
Obama utasababisha kadhia – chukua msafara wa Kikwete zidisha mara 1000! ENDELEA KUSOMA HAPA KWA KUBOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)