Timu mojawapo kutoka Ghana itakayoshiriki Fainali za Pan-African
Guinness Football Challenge Emmanuel Kofi Orkarku na Isaac Aryee
Timu kutoka Kenya Francis Wangari na Kepha Kimani katika picha ya
pamoja na watangazaji wa kipindi cha Guinness Football Challenge Larry
Asego na Mimi kalinda
Waghana Naaab Jonathan Baan na Desmond Odaano, walio na nafasi kubwa yakutwaa ubingwa wa GFC.
Jumatano
iliyopita tarehe 19 Mei 2013 kupitia televisheni za ITV na Clouds TV, timu pinzani kutoka barani
Afrika zilipambana kushindania nafasi mbili za fainali ya mashindano ya
Pan-African GUINNESS® FOOTBALL CHALLEGE™.
Walikuwa ni kutoka Ghana Emanuel Kofi Okarku na Isaac Aryee ambao kwa mara
nyingine walianikiwa kufika katika hatua ya mwisho ya ukuta wa pesa wa Guinness.
Wakenya
katika jezi nyekundu Keneth Muturi na Chris Mwangi walikuwa ni wa kwanza kutoka
baada ya kuwa alama chache zaidi ya timu zingine na kuwa wa mwisho katika
mzunguko wa kwanza wa mchezo. Matumaini ya Afrika mashariki yalirudi baada ya
timu nyingine ya Kenya kukusanya alama 14 katika mzunguko wa pili na kufikia hadi
mzunguko wa penati baada ya kuishinda timu ya Cameroon. Mzunguko wa penati
ulikuwa ni mgumu kwa kuwa timu hizi hazikuachana sana lakini muda ulipokwisha
waghana walishinda na kujipatia dola za kimarekani 4,500 katika hatua ya ukuta wa pesa wa Guinness.
Emmanuel
na Isaac watakutana na Waghana wenzao katika fainali pamoja na washindi wa pili
kutoka Afrika mashariki ambao ni Francis Ngigi na Kepha Kimani na Ephatua
Nyambura na Samuel Papa. Wote wana nafasi ya kupeperusha bendera za nchi zao
lakini watahitaji kujiandaa vizuri ili waweze kuwa washindi wa mashindano haya
ya Guinness Football Challenge.
“Timu zote katika mashindano haya tangu mwanzo
zimefanya vizuri na timu hizi nne za
mwisho zinastahili nafasi ya fainali.Wiki ijayo kutakuwa na mpambano baina ya
Afrika mashariki na Afrika magharibi huku kila upande ukiwa na timu mbili. Tungependa
kuwaomba watu wote kutoka Tanzania Uganda na Kenya kuangalia mchezo huu na
kushangilia timu za Afrika mashariki kuleta taji nyumbani. Timu zote sasa
zitatakiwa kuonesha ujasiri watakapopambana katika fainali ya kwanza kabisa ya
Pan-African Guinness Football Challenge! Usikose kuangalia mchezo huu – hakika itakuwa
ni fainali ya kusisimua”, ....alisema Meneja wa kinywaji cha Guinness, Davis
Kambi.
Wakali
waliotinga fainali za Pan-Afican Guinness Football Challenge:
AFRIKA MASHARIKI:
·
JEZI
ZA KIJANI – kutoka Kenya watakuwa ni Ephatus
Nyambura(24) na Samuel Papa(23).Wtakuwa na matumaini ya kushinda zaidi ya dola
za kimarekeni 3,000 walizopata katika hatua za mwanzo.
·
JEZI
NYEKUNDU – Timu ya pili kutoka Kenya ya Francis
Ngigi(23) na Kepha Kimani(25) kutoka Thika.Timu hii mpaka sasa imejishindia
dola za kimarekani 3,000 na wana matumaini ya kushinda katika fainali.
AFRIKA MAGHARIBI:
·
JEZI
NYEUSI – Emmanuel Kofi Okarku(27) na Isaac
Aryee(25) kutoka Ghana wataichezea timu yao kutoka Afrika magharibi.Tayari wamejishindia
dola 7,000 na wanatarajia kufanya vizuri zaidi katika fainali.
·
JEZI
ZA BLU – Wakubwa walioshinda pesa nyingi zaidi
mpaka sasa ambao ni Jonathan Naab(25) na Desmond Odaano(26) kutoka Larteh
wameshinda hadi dola 20,000.Ni kiasi kikubwa je watafanya vizuri zaidi katika
fainali?
Ushindani
baina ya Afrika mashariki na Afrika magharibi utakuwa ni mkali, nani
atakaeibuka mshindi?
Fainali ya Pan-African Guinness Football Challenge inatayarishwa na kampuni
ya kimataifa ya Endemol na kurushwa katika televisheni ya ITV na Clouds TV
Jumatano saa 3:15 usiku ITV na saa 2:15 usiku Clouds TV. Usikose kushuhudia timu
kutoka Afrika Mashariki ikipambana vikali na nchi zingine za Afrika.
Wapenzi
wa kipindi hiki cha Guinness football challenge barani Afrika wanaweza kupima
maarifa yao katika kabumbu kupitia GUINNESS® VIP™. Wanaweza kufanya hivyo kwa kujisajili bure
kabisa katika m.guinnessvip.com kwa kupitia
simu ya mkononi.
Hakikisha kuufwatilia ukurasa wa facebook wa GUINNESS FOOTBALL
CHALLENGE kwa habari mbalimbali.
-www.facebook.com/guinnesstanzania
Tafadhali kunywa kistaarabu- Hairuhusiwi kuuzwa kwa
wale wenye umri chini ya miaka 18.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)