MKUTANO WA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI NA TANAPA WAENDELEA MKOANI IRINGA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MKUTANO WA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI NA TANAPA WAENDELEA MKOANI IRINGA

1Mkurugenzi wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Allan Kijazi akijibu baadhi ya maswali kutoka kwa washiriki wa mkutano wa wahariri wa vyombo vya habari na TANAPA unaofanyika kwenye ukumbi wa Siasa na Kilimo mjini Iringa ikiwa ni siku ya pili ya mkutano huo, Maada mbalimbali zinawasilishwa leo ikiwa ni pamoja na Masuala ya Utalii ndani ya hifadhi, Miradi ya ujirani mwema na Ulinzi katika mbuga. 2Waziri Kivuli wa Wizara ya Maliasili na Mubnge wa jimbo la Iringa mjini Mchunagji Peter Msigwa akitoa mada katika mkutano huo wakati wa majadiliano kuhusu utalii katika hifadhi za TANAPA kulia ni Mkurugenzi wa Tanapa na Kushoto ni Dr. Ayoub Rioba na mstari wa nyuma kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi Mzingira na Maliasili Ndugu James Lembeli na kushoto ni Meneja uhusiano wa TANAPA Bw. Pascal Shelutete. 3Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi Mzingira na Maliasili Ndugu James Lembeli akizungumza katika mkutano huo unaoendelea mjini Iringa leo 4Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi Mzingira na Maliasili Ndugu James Lembeli akisisitiza jambo wakati akichangia mada katika mkutano huo unaoendelea leo. 5Mhariri wa gazeti la Tanzania Daima Ndugu Charles Misango akiuliza swali katika mkutano huo 6Dr. Ayoub Rioba akiendesha majadiliano katika mkutano huo 7Mwandishi wa habari Antonio Nugas kutoka Radio Clouds kushoto akiwa pamoja na washiriki wengine katika mkutano huo. 8Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mada mbalimbali za mkutano huo. 9Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mada mbalimbali za mkutano huo. 10Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mada mbalimbali za mkutano huo.PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-IRINGA

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages