Mmiliki na Mwendeshaji wa Mtandao Huu Wa Lukaza Blog Mh Josephat Lukaza akiwa katika Kiunga Cha Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOM) juzi alhamisi wakati alipokwenda kufuatilia maswala ya cheti chake.
Kila tarehe 1 JUNE huwa ni siku ya kumbukumbu ya Kuzaliwa kwangu, Leo nakumbuka siku ya kwanza ya safari yangu ya kuingia duniani. Napenda kuchukua nafasi hii Kwanza Kumshukuru Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema ambaye yeye ndie amewezesha hadi mimi Kufika Hapa hii leo
Vilevile Napenda Kuwashukuru Wazazi wangu kwa Kunilea hadi mimi Kufikia hapa nilipo leo Hiyo yote ni kudra za Mwenyezi Mungu Kwa Kuwajalia Nguvu,Upendo na Ustahimilivu wa hali juu na hatimaye Kunifikisha Hapa Nilipo.
Napenda kuchukua Nafasi Hii kuwashukuru Kaka,Dada,Wajomba,Mashangazi,Mashemeji,Binamu,Ndugu, Jamaa na MArafiki zangu Wote kwa kushirikiana na Mimi Katika Kila Hali ya Furaha na Majonzi,Raha na Shida na Naomba tuendelea katika kukuza ushirikiano huu na kupendana KamA Amri Kuu ya Mungu Isemayo "Pendaneni kama Nilivyowapenda mimi"
HAKIKA SIKU YA LEO YA KUMBUKUMBU YA KUZALIWA KWANGU NI SIKU AMBAYO SIYO TU KWASABABU NAZIDI KUZEEKA BALI NI SIKU AMBAYO INAPELEKEA MWAKA HUU KUWA WA MAFANIKIO KWANGU.
HAKIKA MUNGU AKIKUBARIKI HAKUNA WA KUZUIA NA MUNGU AKIKUANDIKIA VYEMA BASI NAPO HAKUNA WA KUZUIA ZAIDI WATACHELEWESHA TU LAKINI UTAIPATA UNACHOSTAHILI. TUZIDI KUMWABUDU MUNGU.
Asante sana Allah........Happy Birthday To Me n Myself,,,,
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)